Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

Manara afunguka anaamini ipo siku atakuja kuwa Rais wa Tanzania

Share

Manara afunguka anaamini ipo siku atakuja kuwa Rais wa Tanzania

Post by Soka Sport on Thu Apr 19, 2018 11:16 am


Afisa Habari wa timu ya soka ya Simba Haji S. Manara, amesema kwamba anaamini kuwa siku moja ndoto yake ya kuwa Rais wa Tanzania itakuja timia, kwani ndio tamanio lake la siku nyingi.

Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa East Africa Television, Haji Manara amesema yeye kama mwanasiasa upande wa pili, ndoto yake kubwa ni kuja kuwa Rais wa nchi baada ya kuzichanga.

“Iko siku mungu akinipa majaliwa, nikazichanga karata zangu, nitakuja kuwa rais, ndiyo ndoto yangu, na ndio ndoto za wanasiasa wote duniani, unaona bunge lile!? kama kuna mwanasiasa ambaye hana ndoto ya kuwa Rais hawafiki watano, mwanasiasa yoyote ukishaingia, hizo ndio ndoto kuja kushika wadhifa wa juu, kama huna ndoto wewe hufai kuishi”, amesema Manara.

Kauli hiyo ya Manara sio mara ya kwanza kusikika akiitamka, huku akisistiza kwamba kwa kuwa yeye ni mwanasiasa mzuri na mkweli, pia ni kada wa CCM, anaamini atakuja kushika wadhifa huo mkubwa kwenye nchi.

Re: Manara afunguka anaamini ipo siku atakuja kuwa Rais wa Tanzania

Post by P. Dybala on Thu Apr 19, 2018 12:29 pm

Sawa kama anavigezo basi ni halali kuwa na ndoto hiyo
King
King
Junior Member

Re: Manara afunguka anaamini ipo siku atakuja kuwa Rais wa Tanzania

Post by King on Thu Apr 19, 2018 1:09 pm

@P. Dybala wrote:Sawa kama anavigezo basi ni halali kuwa na ndoto hiyo
Jamaa huwa anakosa vya kuongea huyo
Hamiliton
Hamiliton
Junior Member

Re: Manara afunguka anaamini ipo siku atakuja kuwa Rais wa Tanzania

Post by Hamiliton on Thu Apr 19, 2018 1:38 pm

anawaza mpira huku anawaza siasa huyu jamaa ni gani?
Payet
Payet
Junior Member

Re: Manara afunguka anaamini ipo siku atakuja kuwa Rais wa Tanzania

Post by Payet on Thu Apr 19, 2018 1:53 pm


Sponsored content

Re: Manara afunguka anaamini ipo siku atakuja kuwa Rais wa Tanzania

Post by Sponsored content


    Current date/time is Fri Feb 22, 2019 5:44 pm