Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

Rais mstaafu Kikwete, Ridhiwani washindwa kuhudhuria harusi ya Ali Kiba

Share

Rais mstaafu Kikwete, Ridhiwani washindwa kuhudhuria harusi ya Ali Kiba

Post by celine dion on Thu Apr 19, 2018 11:54 am

 
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wamesema hawataweza kuhudhuria harusi ya mwanamuziki wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba anayetarajia kufunga ndoa na mchumba wake, Amina Rikesh kutokana na kuwa na majukumu mengine.

Hayo yameleezwa na mtoto wa Rais Kikwete na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwa mjini Dodoma anapohudhuria vikao vya Bunge.

Ridhiwan amesema kuwa, walipewa mwaliko wa kuhudhuria harusi ya mwanamuziki Ali kiba, lakini Rais mstaafu Kikwete kwa sasa anahudhuria shughuli nyingine Marekani, naye Ridhiwani anahudhuria vikao na shughuli mbalimbali bungeni mjini Dodoma hivyo hawataweza kuhudhuria harusi ya mwanamuziki huyo Kenya.

Mwanamuziki Ali Kiba, anatarajia kufunga ndoa kesho na mchumba wake aitwaye Amina Rikesh, alfajiri katika Msikiti wa Ummul Kulthum ulioko eneo la Kizingo, Jijini Mombasa nchini Kenya.

Awali Mama wa bibi harusi mtarajiwa, Asma Said alisema kuwa baada ya ndoa kufungwa itafuatiwa na sherehe ya kupambwa bibi harusi, ambayo itafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini humo.


Chanzo: Mwananchi

    Similar topics

    -

    Current date/time is Fri Feb 22, 2019 5:34 pm