Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

Cristiano Ronaldo ni mchezaji hatari zaidi, takwimu hazidanganyi

LITHIUM
LITHIUM
New Member
New Member

Cristiano Ronaldo ni mchezaji hatari zaidi, takwimu hazidanganyi Empty Cristiano Ronaldo ni mchezaji hatari zaidi, takwimu hazidanganyi

Post by LITHIUM on Mon Apr 09, 2018 4:05 pm

Ronaldo anaongoza orodha wachezaji wenye magoli mengi katika michuano yote ya Ulaya!

1. Cristiano: 120
2. Messi: 101
3. Raul: 76
4. Inzaghi: 70
5. Muller: 69

Katika la liga Ronaldo kafunga magoli 300 katika mechi 286

Pia ndie mfungaji was Madrid wa muda wote.
kafunga zaidi mabao 324 kwenye mechi 310 kaivunja rekodi ya Raul Gonzalez ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid, lakini alitumia mechi 741 kufunga mabao 323.

Huyo ndio mnyama Christiano Ronaldo.


Cristiano Ronaldo ni mchezaji hatari zaidi, takwimu hazidanganyi Images11Ni Cristiano Ronaldo tena anaendelea kuwanyamazisha wapinzani wa Real Madrid, dakika ya 3 tu alipiga shuti lake la 9 kwa Gianluigi Buffon na kufunga bao lake la 8 dhidi ya golikipa huyo, hili likiwa bao la kwanza katika mchezo huu.

Dakika ya 64 Cristiano Ronaldo tena aliifungia Real Madrid bao la pili na kumfanya kuwa mchezaji katika historia aliyewafunga Juve mabao mengi (9) kabla ya Marcelo kufungia bao la 3 Real Madrid.

[​IMG]Hii ni mara ya kwanza Juventus wanaruhusu kufungwa mabao 3 nyumbani tangu mwaka 2009 walipofungwa bao 4-1 na Bayern Munich, Juventus walimaliza wakiwa pungufu baada ya Paulo Dyabala kuoneshwa kadi nyekundu.

Kama hujui tu ni kwamba bao la kwanza la Madrid ndio bao la mapema zaidi kwa Cristiano Ronaldo kuwahi kufunga katika Champions League, huku sasa Mreno huyo akiwa na mabao 38 katika msimu huu(michuano yote) ikiwa ni idadi kubwa kuliko mchezaji yeyote barani Ulaya.

Tangu klabu ya Juventus wahamie katika uwanja wao mpya mwaka 2011 hawajawahi kupokea kipigo kama hiki katika uwanja huo katika mashindano yoyote yale
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 10:42 pm