Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo

YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo Empty YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo

Post by Roy on Fri Apr 06, 2018 10:45 am

YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo Woliat10

Kocha mkuu wa klabu ya Zimamoto ya Zanzibar ambaye pia ni mkurugenzi wa ufundi wa chama cha soka Zanzibar (ZFA) adbulan Msoma ametoa ushauri wa bure kwa Yanga kuhusu wapinzani wao Wolaitta Dicha kabla ya mechi yao ya kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika.

Msoma anaifahamu Wolaitta Dicha baada ya kucheza na timu yake msimu huu lakini Zimamoto iliondoshwa kwenye mashindano baada ya kufungana 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Zanzibar kabla ya kufunga 1-0 kwenye mechi ya marudiano huko Ethiopia.

“Wolaitta Dicha kwa uzoefu wangu wa kufundisha timu zilizocheza mashindano ya Afrika, ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo lakini maajabu ni kuona imefika hadi hatua hii.”

“Ni timu ambayo inategemea wachezaji wawili (nahodha wao ana rasta na kiungo mmoja anatumia mguu wa kushoto anavaa jezi namba 17) hao wanaweza kuwa tishio kwa timu yoyote.”

“Wachezaji wengine ni wa kawaida kabisa tena dhaifu kabisa, walinzi si wazuri kwa vichwa hawaangalii watu wanaangalia mpira ni suala la kufunga magoli tu, mie nimekosa magoli manne hapa Unguja na kule kwao nimegongesha mwamba mara mbili kwa sababu si wachezaji wanaojua kikamilifu wanachofanya uwanjani.”

“Ni wazuri kwa pasi fupifupi kwenye eneo la kiungo kwa hiyo kama mnafata mpira watawapita, lakini kama timu inawashambulia wanakuwa hawana la kufanya. Halafu ni timu dhaifu pembeni kwa hiyo nafasi ya timu kama Yanga naiona ni kubwa ikiwa watatumia mapungufu hayo.”

“Kiufundi waende mapema kwa sababu Ethiopia ipo juu na wale hawapo Addis Ababa wapo Awasa, wakifika Addis Ababa labda watalala siku moja halafu watasafiri kwa ndege kwa muda wa nusu saa wanafika kwenye huo mji wao.”

“Uwanja sio mzuri (pitch) kwa hiyo waende mapema kama siku nne au tatu wapate uzoefu wa hali ya hewa.”

YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo Empty Re: YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo

Post by Roy on Fri Apr 06, 2018 10:46 am

Very Happy Very Happy Very Happy Very Happy Very Happy Very Happy Very Happy Very Happy Very Happy

YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo Empty Re: YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo

Post by Roy on Fri Apr 06, 2018 6:04 pm

sawa
ramsey
ramsey
Junior Member

YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo Empty Re: YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo

Post by ramsey on Sun Apr 08, 2018 10:23 am

YEBOYEBO bounce bounce bounce bounce

Sponsored content

YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo Empty Re: YEBOYEBO yapewa mbinu kuwamaliza waethiopia “Ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo

Post by Sponsored content

  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 10:31 pm