Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

Rasmi Lwandamina kocha mpya Zesco

Nani
Nani
Junior Member

Rasmi Lwandamina kocha mpya Zesco Empty Rasmi Lwandamina kocha mpya Zesco

Post by Nani on Tue Apr 10, 2018 11:29 pm

Mabingwa wa Zambia, Zesco wamemtangaza rasmi kocha George Lwandamina kuwa kocha wao mpya.

Lwandamina ambaye bado ana mkataba na Yanga, ameondoka bila ya kuaga na Yanga hawakuwa wakijua alipo.

Lakini Kocha huyo, ametangazwa leo rasmi kurejea kwa Zambia na kujiunga na klabu yake hiyo ambayo aliiacha na kujiunga na Yanga.

Mabingwa hao wa Zambia, wamesema wameishamalizana na Lwandamina na ataanza kazi mwezi ujao.

Aliyekuwa Kocha wa Zesco, Tenant Chembo aliamua kuachia ngazi na Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo, Richard Mulenga anaonekana ndiye alifanya juu chini kuhakikisha Lwandamina anarejea.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo jioni, Zesco imesema imeamua kumrejesha Lwandamina kutokana na ubora na weledi wake kwa lengo la kuendelea kuijenga zaidi kwa upande wa wachezaji na kuboresha umoja kati ya uongoza, wanachama na mashabiki wao.

Wakati kocha mkuu amejiuzulu, msaidizi wake Emmanuel Siwale ndiye ataiongoza Zesco kesho dhidi ya Lusaka Dynamo.
mikael
mikael
Junior Member

Rasmi Lwandamina kocha mpya Zesco Empty Re: Rasmi Lwandamina kocha mpya Zesco

Post by mikael on Wed Apr 11, 2018 9:54 am

Lwandamina ni mpumbafu sana
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 11:06 pm