Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

MZEE MAJUTO ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI?

MZEE MAJUTO  ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI? Empty MZEE MAJUTO ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI?

Post by Dele Alli on Wed Apr 11, 2018 1:47 am

Siku chache baada ya kufanyika kwa tuzo za Filamu zinazojulikana kama Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) na mrembo Wema Sepetu kuibuka mshindi kwa upande wa waigizaji wa kike, msanii mkongwe nchini Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ amesema mrembo huyo hawezi kuwa mkali kushinda Riyama Ally.

Katika kipengele hicho Wema alikuwa akichuana na wasanii nane na filamu walizoigiza kwenye mabano akiwemo Getrude Mwita (Bantu), Rachel Kayuga (Safari ya Gwalu), Aisha Mwajumla (Watatu), Riyama Ali (Mama wa Marehemu).

Wengine ni Amina Rashid (Bandidu), Hawa Abeid (Genge), Sharifa Mansury (Kivuli cha ahadi) na Neema Mangowi (Malaika) wakati Wema yeye aliingia kupitia filamu yake ya Heven Sent.

Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 4, Mzee Majuto amesema kwake bado Riyama ni mkali na hawezi kufananishwa na Wema katika kuuvaa uhusika anapokuwa mbele ya kamera.

“Mimi nimekaa kwenye fani hii ya uigizaji siku nyingi, najua nani mwigizaji nani amevamia fani japo najua kuna watu wataniponda, lakini ukweli Riyama alistahili kubeba tuzo ile na sio Wema,” amesema msanii huyo anayewavunja watu mbavu kwa vichekesho.

Pia ametaja sababu ambazo ameona ndizo zilizomwezesha Wema kushinda kuwa zimetokana na mambo ya kidijitali, kwa yeye kuwa na mashabiki wengi mtandaoni ambao waliweza kumpigia kura tofauti na wasanii wengine alioshindanishwa nao.

Katika ushauri wake, Mzee Majuto amesema ni vizuri wakati mwingine majaji wasiangalie hilo la upigaji kura na badala yake waangalie vipaji vya watu kwani kwa kufanya hivyo itawavunja moyo wengine wanaotaka kufanya vizuri kwa kuona tayari wana washindi wao mfukoni.

Hata hivyo kwa upande wa msanii bora wa kiume, Mzee Majuto amesema Ahmed Salim ’Gabo’ amestahili kwa kuwa hakuna asiyejua kipaji cha msanii huyo tangu alivyoanza kung’ara kwenye filamu mbalimbali alizoigiza.

Katika tuzo hizo, vipengele 19 vilikuwa vikishindaniwa, ambapo kwa washindi bora wa kike na kiume kila mmoja aliondoka na tuzo na Sh5 milioni taslimu, wakati vipengele vingine walipata Sh1 milioni.

Unafikiri mzee majuto yuko sahihi?

MZEE MAJUTO  ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI? Empty Re: MZEE MAJUTO ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI?

Post by celine dion on Wed Apr 11, 2018 10:14 am

ni kweli
Anonymous
selunkuma
Guest

MZEE MAJUTO  ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI? Empty Re: MZEE MAJUTO ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI?

Post by selunkuma on Thu Apr 12, 2018 11:50 am

hata mimi nilishangaa
James Kub
James Kub
Junior Member

MZEE MAJUTO  ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI? Empty Re: MZEE MAJUTO ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI?

Post by James Kub on Thu Apr 12, 2018 5:54 pm

yuko sawa mzee

MZEE MAJUTO  ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI? Empty Re: MZEE MAJUTO ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI?

Post by Roy on Sun Apr 15, 2018 5:56 pm

na huo ndio ukweli

Sponsored content

MZEE MAJUTO  ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI? Empty Re: MZEE MAJUTO ANASEMA WEMA SEPETU AWEZI KUWA MKALI KUSHINDA RIHAMA JE NI KWELI?

Post by Sponsored content

  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 11:34 pm