Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

WAKATI WANAPAMBANA NA SIMBA, WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAIBIWA VITU HOTELI

Chuga
Chuga
New Member
New Member

WAKATI WANAPAMBANA NA SIMBA, WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAIBIWA VITU HOTELI Empty WAKATI WANAPAMBANA NA SIMBA, WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAIBIWA VITU HOTELI

Post by Chuga on Wed Apr 11, 2018 5:02 am

Wakati wachezaji wa Mtibwa Sugar wakiwa uwanjani wakipambana na Simba, vibaka ambao wanaaminika ni wafanyakazi wa hoteli waliyokuwa wamefikia mjini Morogoro, walikuwa wakifanya kazi yao ya wizi.

Wachezaji wa Mtibwa Sugar wameibiwa vifaa vyao mbalimbali na tayari uongozi wao umethibitisha ukisema kipa Shabani Kado aliyekuwa katika benchi siku hiyo Mtibwa ikilala 1-0, ndiye ameathirika zaidi.

Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema wanaamini baadhi ya wafanyakazi wa hoteli hiyo ndiyo wamecheza mchezo huo mchafu.

“Kwa kweli ni jambo baya sana, Kado ndiyo kaibiwa vitu vya zaidi ya shilindi laki tatu. Tayari tumefungua kasi kituo cha polisi na wametupa ushirikiano mkubwa sana.

“Juhudi za kuwasaka wahalifu zimefanyika na baadhi wameishakamatwa na uchunguzi unaendelea,” alisema Kifaru.

“Tuligundua kuna matatizo baada ya kurejea hotelini tukitokea uwanjani katika mechi ya Simba. Baada ya hapo tukagundua pia hakukuwa kumevunjwa, maana yake walifungua na ufunguo na kuiba katika vyumba mbalimbali.

“Mfano kuna simu, ipad, kompyuta na vitu vingine vya gharama. Ni jambo baya sana hili,” alisisitiza Kifaru akizungumza na SALEHJEMBE.

WAKATI WANAPAMBANA NA SIMBA, WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAIBIWA VITU HOTELI Empty Re: WAKATI WANAPAMBANA NA SIMBA, WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAIBIWA VITU HOTELI

Post by celine dion on Sun Apr 15, 2018 6:02 pm

Wink Wink Wink
rosee
rosee
New Member
New Member

WAKATI WANAPAMBANA NA SIMBA, WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAIBIWA VITU HOTELI Empty Re: WAKATI WANAPAMBANA NA SIMBA, WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAIBIWA VITU HOTELI

Post by rosee on Fri Apr 20, 2018 1:29 am

hakua ulinzi?

Sponsored content

WAKATI WANAPAMBANA NA SIMBA, WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAIBIWA VITU HOTELI Empty Re: WAKATI WANAPAMBANA NA SIMBA, WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAIBIWA VITU HOTELI

Post by Sponsored content

  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 10:30 pm