Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

REAL MADRID YAFUZU HATUA YA NUSU FAINALI ''KWAMBINDE''

Naija
Naija
New Member
New Member

REAL MADRID YAFUZU HATUA YA NUSU FAINALI ''KWAMBINDE''  Empty REAL MADRID YAFUZU HATUA YA NUSU FAINALI ''KWAMBINDE''

Post by Naija on Thu Apr 12, 2018 10:54 am

ISPANIA: Miamba ya Hispania Real Madrid jana imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya kupata penati liyokuwa na utata mkubwa iliyozusha tafrani za wachezeaji wa Juve na refarii muingereza Michael Oliver.

Penati hiyo ilikuja baada ya Medhi Benatia katika mazingira yenye utata kumdondosha na Lukas Vazquez kwenye eneo la hatari ndipo Refa huyo kuamua kutenga tuta lilopigwa na mshambuliaji wa Ureno Christian Ronald katika dakika za majeruhi,Ni katika mazingira hayo hayo, kwa kile kilichosemwa kuwa ni matumizi ya lugha mbaya, mlinda mlango wa Juve, Gianluigi Buffon katika ile ambayo inaweza kuwa Champions League yake ya mwisho alitupwa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi huyo, kadi ambayo nayo imeleta utata kwa sababu Buffon kama kiongozi wa timu yaani kepteni anahaki ya kwenda kulalamikia penati ile.Real, washindi mara tatu wa Ligi ya mabingwa Ulaya katika misimu minne, waliingia katika mechi hiyo ya mzunguko wa pili wakiongoza kwa mabao 3-0 lakini viongozi hao wa Seria A walianza kupoteza matumaini pale Mario Mandzukic aliposukuma kichwa nyavuni kutoka kwenye mkwaju ulionyunyizwa na Sami Khedira dakika mbili tu tangu kuanza kwa mchezo. Huyo huyo Mandzukic akapata goli la pili kupitia kichwa muda mfupi kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza.Blaise Matuidi akafunga la tatu kutokana na makosa yaliyofanywa na Keylor Navas na hivyo kuifanya Juventus iwe na matokeo sawa na Real Madrid, jambo ambalo lingeipeleka mechi katika dakika za nyongeza kama siyo tukio la Penati lililotokea na kuifanya Real Madrid kutinga nusu fainali katika mazingira ambayo mashabiki wao walikuwa tayari wamekata tamaa.Sasa, Real inaungana na Liverpool, Roma na Bayern katika droo ya timu nne zilizosalia, droo itakayofanyika Nyon, Uswisi, Ijumaa.

Bayern wao wametinga nusu fainali kwa maara ya saba katika miaka tisa baada ya kumaliza mechi yao dhidi ya Sevilla kwa matokeo ya bila kufungana lakini wakiwa na magoli mawili kibindoni dhi ya moja la Sevilla katika mechi ya mzunguko wa kwanza.
mikael
mikael
Junior Member

REAL MADRID YAFUZU HATUA YA NUSU FAINALI ''KWAMBINDE''  Empty Re: REAL MADRID YAFUZU HATUA YA NUSU FAINALI ''KWAMBINDE''

Post by mikael on Thu Apr 12, 2018 12:43 pm

na ndiye ananyanyua ndoo
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 10:27 pm