Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

Aunt Ezekiel asema hakuna sababu ya kulia kila siku kifo cha Kanumba

Anonymous
Martin salvatory
Guest

Aunt Ezekiel asema hakuna sababu ya kulia kila siku kifo cha Kanumba Empty Aunt Ezekiel asema hakuna sababu ya kulia kila siku kifo cha Kanumba

Post by Martin salvatory on Thu Apr 12, 2018 11:06 am

STAA wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa hakuna sababu ya kulia kila siku kuhusiana na kifo cha aliyekuwa staa wa filamu Steven Kanumba, badala yake waige mfano wake ili tasnia hiyo izidi kusonga mbele.

Akizungumza na gazeti hili, Aunt alisema mara nyingi wasanii wanapoadhimisha kumbukumbu ya kifo chake, wanakuwa wanalia au wengine wanasononeka mara kwa mara hiyo inakuwa inazidi kurudisha tasnia nyuma badala yake wasanii wakaze buti waweze kufika alipokuwa amefika yeye.

“Najua wazi uchungu upo lakini inabidi tuache sasa kulia badala yake tujitahidi kufikia pale alipotuacha ili tuzidi kusonga mbele maana tukisema kulia kila siku hatuwezi kufika tunapotaka hata siku moja,” alisema Aunt.
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 10:28 pm