Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

ROBERTO FIRMINO ANAVYOFURAHI KUTUDANGANYA.

Kun
Kun"
Junior Member

ROBERTO FIRMINO ANAVYOFURAHI KUTUDANGANYA. Empty ROBERTO FIRMINO ANAVYOFURAHI KUTUDANGANYA.

Post by Kun" on Thu Apr 12, 2018 12:30 pm

Umemuona Roberto Firmino yule Mbrazil anayesimama katikati kwenye ule utatu mtakatifu wa Sadio Mane, Firmino na Mohammed Salah pale Liverpool?. Kwenye viunga vya Merseyside mashabiki na wachezaji wenzake wanamuita "Bobby" wakifupisha jina lake la Roberto.

Bobby yupo kwenye kiwango bora sana kwa sasa, yeye pamoja na Mane na Salah wamefanikiwa kutengeneza kombinesheni ya hatari sana inayoogopwa si tu na mabeki nchini England bali hata mabeki wengine kwenye club za barani Ulaya. Wanawaogopa sana hawa kina Bobby. Mane, Bobby na Salah wanafunga kadiri wanavyojisikia, haiwezi pita mechi kama mmoja, wawili ama wote watatu kufunga. Hawa ndio sababu kuu ya mafanikio wanayoyapata Liverpool msimu huu.

Mane tunamuelewa, Salah hana shida kabisa anaeleweka, tatizo ni huyu Bobby. Bobby anatunganya sana. Kwa wale ambao hawamfahamu hawatoona utofauti, ila sisi tunaomfahamu vizuri tunaamini kabisa anatunganya.

Tangu mwanzo kabisa mara baada ya kuwasili kwa Mohammed Salah, hapo Bobby ndipo alipoanza kutunganya rasmi... Aliamua kufanya kitendo cha kiungwana kabisa cha kumuachia Salah jezi namba 11 na yeye kuvaa jezi namba 9. Huo ulikua ni uongo wake wa kwanza.. Hapo Bobby alitaka atuaminishe kwamba yeye ni mshambuliaji wa kati, wakati sisi tunaomfahamu tunajua kwamba hiyo si nafasi yake halisi uwanjani.

Mwaka 2005 wakati Kocha Luciano Spalletti akianza kuifundisha club ya AS Roma ya nchini Italy alimfanya Francesco Totti atudanganye pia. Spalletti alianza kumtumia Totti kama mshambuliaji wa kati ingawaje hiyo haikuwa nafasi yake rasmi. Totti alizoeleka kucheza kama kiungo mshambuliaji anayesimama nyuma ya mshambuliaji ama kama winga anayetokea pembeni.

Totti alikua bora akicheza kama kiungo mshambuliaji, ila kitendo cha Spaletti kumbadilisha na kumchezesha kama mshambuliaji wa kati kulimfanya akawa bora zaidi.. Tofauti na ilivyokua mwanzoni, Totti akawa anafunga magoli mengi huku pia akifurahia kuichezesha timu kwa kutoa pasi nyingi za magoli. Msimu wa mwaka 2006/2007 ndiye alikua mfungaji bora wa ligi kuu nchini Italy.

Kama ilivyokua kwa Totti, Roberto Firmino nae alikua ni kiungo mshambuliaji mzuri tu ambaye wakati mwingine alikua akicheza kama winga wa pembeni tangu akiwa kwao nchini Brazil kwenye club ya Figueirense na hata Ujerumani kwenye club ya 1899 Hoffenheim. Bobby alikua bora kwenye nafasi hiyo, alikua akifunga na kutoa pasi za magoli. Mwaka 2014 alikua bora sana, club nyingi za England zikiwemo Man United, Liverpool na Arsenal zilivutiwa nae, kila mmoja ikihitaji huduma yake.

23 June 2015, Liverpool walikubali kulipa ada ya £29M kwa ajili ya kumsajili Bobby. Mwanzoni ndani ya maisha mapya na Liverpool aliendelea kucheza katika nafasi zake zilizile, kama kiungo mshambuliaji ama winga wakati mwingine.

Ujio wa Salah na uwepo wa Mane, ukamfanya Bobby awe anatumika zaidi kama mshambuliaji wa kati. Bobby ni mjanja-mjanja, pamoja na kucheza katikati tena akiwa na jezi yake namba tisa mgongoni, amekua anawadanganya sana mabeki, hachezi kwa kukaa kusubiri mpira sehemu moja kama ilivyo kwa Lukaku, Morata ama washambuliaji wengine wa kati, yeye huzunguka kushoto, kulia ama kushuka chini kwa viungo wake.

Ujanja huu ndio umemfanya awadanganye zaidi mabeki na kumpa faida ya kufunga magoli mengi kadiri atakavyo huku pia akitumia vizuri nafasi yake kama kiungo mshambuliaji kwa kutoa pasi za magoli. Bobby yupo kwenye kiwango bora sana kwa sasa. Yeye ndiye anayemfuatia Cristiano Ronaldo kwenye orodha ya wafungaji UEFA Champions League akiwa na magoli saba... Huku kwenye premier league ana magoli 12.

Siku zote Bobby amekua akifurahi kutudanganya. Huwa anafunga huku anatabasamu, anashangilia goli huku anatabasamu... Anatabasamu kwa sababu ya furaha yake kuwadanganya mabeki wanaomsahau.. Anatabasamu kwa sababu anatunganya sisi ambao hatukumuona kama anaweza kucheza vizuri akiwa mshambuliaji wa kati.

Wachezaji kama Bobby ndio wanahitajika sana kwenye kikosi kwani wanauwezo wa kukupa options nyingi uwanjani. Ni kama vile Lionel Messi anavyokua na options nyingi kwa kucheza nafasi tofauti tofauti uwanjani. Yawezekana kwa sasa Bobby yupo anaogolea kwenye swimming pool huku akiendela kutabasamu kwa kadiri anavyotunganya kila siku. Siku zote nmekua nikifurahi sana kumuona uwanjani akicheza na hasa kama atafunga goli, kuna namna jinsi anavyoshangilia magoli yake huwa napenda sana.
mikael
mikael
Junior Member

ROBERTO FIRMINO ANAVYOFURAHI KUTUDANGANYA. Empty Re: ROBERTO FIRMINO ANAVYOFURAHI KUTUDANGANYA.

Post by mikael on Thu Apr 12, 2018 12:41 pm

Itabd ww uwe shaffih na shaffih angekua ww
moyo
moyo
New Member
New Member

ROBERTO FIRMINO ANAVYOFURAHI KUTUDANGANYA. Empty Re: ROBERTO FIRMINO ANAVYOFURAHI KUTUDANGANYA.

Post by moyo on Thu Apr 12, 2018 12:51 pm

hivi huyu Bobby na Sarah walikuwepo kwenye match ya MANCHESTER UNITED VS Liverpool

Sponsored content

ROBERTO FIRMINO ANAVYOFURAHI KUTUDANGANYA. Empty Re: ROBERTO FIRMINO ANAVYOFURAHI KUTUDANGANYA.

Post by Sponsored content


    Current date/time is Mon Jul 22, 2019 7:16 pm