Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

Ikiwa bado siku twende Escape One “Mo Salah shakani Marseyside Derby”

Ikiwa bado siku twende Escape One “Mo Salah shakani Marseyside Derby” Empty Ikiwa bado siku twende Escape One “Mo Salah shakani Marseyside Derby”

Post by Roy on Fri Apr 06, 2018 1:51 pm

Imebaki siku moja tu kwa ile siku kubwa sana katika EPL kufika, ni kesho ambapo ukiacha derby kati ya Manchester City na Manchester United, kutakuwa na ile Marseyside derby kati ya Liverpool na Everton na zote tutaziangalia pale Escape One.

Liverpool wametoka kuwapiga Man City bao 3 katika Champions League lakini hii sio habari inahoiathiri Marseyside derby, ugumu wa mchezo huu bado uko pale pale kama ulivyo wakati wowote ule.

Ikiwa bado siku twende Escape One “Mo Salah shakani Marseyside Derby” Img_2010

Hofu imetanda katika upande wa Liverpool baada ya mchezaji wao tegemezi Mohamed Salah kupatwa na majeruhi ya kifundo cha miguu, ambayo inadaiwa kwamba alicheza nayo katika mchezo dhidi ya City.

Jana katika viunga vya karibu na uwanja wa Anfield Salah alionekana akiingia hospitali na hili lilizidi kuleta maswali kwa mashabiki wengi wa Liverpool kama mchezaji huyo atakuwepo uwanjani siku ya kesho ama laa.

Siku ya jana Salah hakuweza kufanya mazoezi na timu kwani alipofika uwanjani madaktari walishauri asifanye mazoezi bali aende kafanyiwe scanning kuangalia ukubwa wa tatizo lake.

Nje ya hospitali mashabiki wengi wa Liverpool walikuwa wakimuuliza Mo Salah kama ataweza kuvaa jezi Jumamosi na kucheza dhidi ya Everton lakini mchezaji huyo hakuwa na jibu la moja kwa moja zaidi ya kutabasamu tu na kutikisa mabega akiashiria hajui.

Kwa upande wa kocha wa Liverpool amesema Salah hana majeraha makubwa na mechi yao na City ilipoisha alisema yuko fiti, lakini bado kunasubiriwa taarifa kamili kutoka kwa madaktari kuhusu hali ya Salah.
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 10:54 pm