Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

BUFFON AMCHARUKIA MWAMUZI MWINGEREZA, ASEMA HANA MOYO KIFUANI, AMFANANISHA NA MUUAJI

Share

BUFFON AMCHARUKIA MWAMUZI MWINGEREZA, ASEMA HANA MOYO KIFUANI, AMFANANISHA NA MUUAJI

Post by Roy on Thu Apr 12, 2018 4:47 pm

Kipa mkongwe nchini Italia, Gianluigi Buffon ameamsha mashambulizi dhidi ya mwamuzi Michael Oliver kwa kumuita muuaji.

Kama haitoshi, Buffon amesema mwamuzi huyo hana moyo katika kifua chake.

Mara baada ya Juventus kurejea kwa Italia, Buffon amesema Oliver kutoka Uingereza ameipendelea waziwazi Real Madrid kwa kuipa mkwaju wa penalti ambao hawakustahili.

Juventus iliitwanga Madrid kwa mabao 3-1 kwao Santiago Bernabeu lakini ikang’oka katika hatua hiyo ya robo fainali kutokana na bao la mkwaju wa penalti waliopata Madrid katika dakika za nyongeza.

Mwamuzi alipuliza filimbi kuashiria faulo baada ya Lucas Vazquez kuamgushwa katika dakika ya 90+3.

Baada ya maneno makali, Buffon alitolewa nje kwa kadi nyekundu jambo ambalo lilizidisha hasira za mashabiki wa Juventus na wale wasioiunga mkono Madrid.
Anonymous
alli
Guest

Re: BUFFON AMCHARUKIA MWAMUZI MWINGEREZA, ASEMA HANA MOYO KIFUANI, AMFANANISHA NA MUUAJI

Post by alli on Fri Apr 13, 2018 6:21 pm

buffon hana bahati bora astafu tu soka

Re: BUFFON AMCHARUKIA MWAMUZI MWINGEREZA, ASEMA HANA MOYO KIFUANI, AMFANANISHA NA MUUAJI

Post by Roy on Fri Apr 13, 2018 8:18 pm

alli wrote:buffon hana bahati bora astafu tu soka

mwenye bahgati ni nani?
Payet
Payet
Junior Member

Re: BUFFON AMCHARUKIA MWAMUZI MWINGEREZA, ASEMA HANA MOYO KIFUANI, AMFANANISHA NA MUUAJI

Post by Payet on Fri Apr 13, 2018 8:23 pm

Refaree alizingua sana

Sponsored content

Re: BUFFON AMCHARUKIA MWAMUZI MWINGEREZA, ASEMA HANA MOYO KIFUANI, AMFANANISHA NA MUUAJI

Post by Sponsored content

    Current date/time is Fri Feb 22, 2019 5:40 pm