Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

MASHABIKI YANGA WAVAMIA MAKAO MAKUU YA KLABU USIKU HUU KUMSAKA MKWASA, SABABU NI LWANDAMINA

Share

MASHABIKI YANGA WAVAMIA MAKAO MAKUU YA KLABU USIKU HUU KUMSAKA MKWASA, SABABU NI LWANDAMINA

Post by Mavugo R on Thu Apr 12, 2018 6:03 pmBaadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga wamevamia ofisi za Makao Makuu ya klabu hiyo usiku huu wakimtaka Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwasa.

Mashabiki wamejitokeza Makao Makuu ya klabu wakimtamka Mkwasa awape ufafanuzi kuhusiana na kuondoka kwa Kocha George Lwandamina ambaye amerejea kwa Zambia kujiunga na timu yake ya zamani, Zesco United.

Baada ya kuwasili ofisini hapo, wengi wameonekana wakimtupia lawama Mkwasa, wakisema kuwa yeye ndiye chanzo cha kuondoka kwa Lwandamina kimyakimya.

Taarifa zilizoripotiwa baada ya kuondoka kwa Lwandamina, zinaeleza kuwa Mkwasa na Kocha huyo hawakuwa na maelewano mazuri haswa katika masuala mazima ya utendaji.

Mbali na utendaji, inaelezwa pia Mkwasa ana mpango wa kuachana na wadhifa wa Ukatibu Mkuu ili kuchukua nafasi ya Lwandamina.

    Current date/time is Fri Feb 22, 2019 5:35 pm