Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu Empty UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

Post by bakayoko chelsea on Fri Apr 13, 2018 10:22 am

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu Images?q=tbn:ANd9GcRcxBwf34ZukjxurR4gHDGQK-153urmpLLW3f4D9yx-jWNK4YY3

Katika msimu wa 2003/2004 wa Uefa champions league hatua ya robo fainali, deportivo ilipigwa goli 4-1 katika mechi ya kwanza na timu iliyokuwa Moto wakati huo, Ac Milan ya Anceloti pale katika dimba la San Siro Italia. Katika mechi ya marudiano dimba la Riazor, Spain, Anceloti na Jeshi lake waliamini kwamba wana kazi ndogo sana ya kumalizia, kwani kwa hakika hakuna timu hata moja ambayo iliwahi kupindua matokeo ya aina ile katika michuano ya Uefa. Ilichukua dakika 5 tu baada ya kipenga, Walter Pandiani akampga chenga ya kumgeuza mtu mzima, Paolo Maldini, na kumimina mkwaju mkali ambao golikipa Dida hakuuona. Deportivo walizidi kupapasa soka balaa, ambapo kwa kifupi tu, hadi mapumziko walikuwa wakiongoza 3 bila, kipindi cha pili wakapga la 4, na kuitoa Milan kwa 5-4. Hadi mechi inaisha Anceloti hakuamini kilichokuwa kikitokea mbele ya macho yake, akaamini huenda anaota. Pamoja na kuwa na washambuaji walafi wa magoli kama Filipo Inzagi na Rui Costa, akajikuta akitupwa nje ya michuano hii.

Vikosi vilikuwa hivi.
Deportivo la Coruna.
Jose Francisco Molina (GK), Manuel Pablo, Enrique Romero, Nourredine Naybet, Mauro Silva (C),Walter Pandiani,Sergio Gonzalez, Jorge Andrade, Sanchez Victor, Albert Luque na Juan Carlos Valeron.

Ac Milan.
Dida (GK),Cafu, Paolo Maldini (C),Andry Chevchenko,Genaro Gattuso, Alessandro Nesta, Joh Dahl Tomasson, Clarence Seedorf, Andrea Pirlo, Ricardo Kaka na Giussepe Pancaro.
Anonymous
ismail
Guest

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu Empty Re: UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

Post by ismail on Fri Apr 13, 2018 11:35 am

hebu tueleze na maajabu waliyofanya majogoo wa anfield dhidi ya AC MILAN!
Anonymous
TUMAIN
Guest

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu Empty Re: UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

Post by TUMAIN on Fri Apr 13, 2018 11:39 am

mbona Kawaida sana

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu Empty Re: UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

Post by Roy on Fri Apr 13, 2018 1:55 pm

sawa ila mbona timu nyingi hufanya hayo maajabu
CR7
CR7
Junior Member

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu Empty Re: UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

Post by CR7 on Fri Apr 13, 2018 4:06 pm

maajabu yako wapi hapo

Payet
Payet
Junior Member

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu Empty Re: UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

Post by Payet on Fri Apr 13, 2018 8:29 pm

ismail wrote:hebu tueleze na maajabu waliyofanya majogoo wa anfield dhidi ya AC MILAN!

kweli bwana yale ndo yalikuaga maajabu ya soka
lallana
lallana
New Member
New Member

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu Empty Re: UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

Post by lallana on Fri Apr 13, 2018 8:37 pm

ismail wrote:hebu tueleze na maajabu waliyofanya majogoo wa anfield dhidi ya AC MILAN!

yaa hakika yale ndo maajabu ya soka

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu Empty Re: UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

Post by Mkweli daima on Fri Apr 13, 2018 9:12 pm

unataka kusemaje?

Sponsored content

UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu Empty Re: UCL: Deportivo la Coruna, timu iliyowahi kufanya maajabu

Post by Sponsored content

  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 11:23 pm