Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

Rais mstaafu Dr. Kikwete ajitolea kumsaidia Mzee Majuto matibabu India, pia kumnunulia trekta la kilimo

Rais mstaafu Dr. Kikwete ajitolea kumsaidia Mzee Majuto matibabu India, pia kumnunulia trekta la kilimo Empty Rais mstaafu Dr. Kikwete ajitolea kumsaidia Mzee Majuto matibabu India, pia kumnunulia trekta la kilimo

Post by bakayoko chelsea on Fri Apr 13, 2018 10:25 am

Rais mstaafu Dr. Kikwete ajitolea kumsaidia Mzee Majuto matibabu India, pia kumnunulia trekta la kilimo KIKWETE

LICHA ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume bado hali ya staa wa filamu za Kibongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ni tete ambapo Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, amejitosa baada ya kumuona alivyodhoofu kwa sasa.

JK na Mzee Majuto walikutana uso kwa uso wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar katika Tuzo za Kimataifa za Sinema Zetu ambapo walionekana wakiteta kwa dakika kadhaa kabla ya kila mmoja akaenda kukaa kwenye siti yake.

Hali ya mzee Majuto haikuonekana nzuri na alionekana ukumbini akitembea kwa msaada wa fimbo huku akionekana kutokuwa mchangamfu kama ilivyo kawaida yake, hali iliyowahuzunisha mashabiki wake waliokuwa ukumbini hapo.

Baada ya mazungumzo hayo Mzee Majuto amesema kuwa, kutokana na hali yake kutokuwa nzuri licha ya kufanyiwa upasuaji, Muheshimiwa JK amemuahidi kwamba watajadili na Rais Magufuli na ili wampeleke India kwa matibabu zaidi kwani tiba za hapa hajaridhishwa nazo.

“JK ameniahidi kwamba watanipeleka India kwa ajili ya matibabu ikiwa ni baada ya kwenda na kujadili na rais aliyeko madarakani Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ ili nikapate matibabu zaidi maana tiba nilizopatiwa hapa bado sijakaa sawa.

“Kwanza kwa sasa nimepatwa ugonjwa mpya tena ambapo mkono unaniuma mno, ninashindwa hata kushika chochote ndiyo nataka nirudi tena hospitalini nikawaeleze kuhusu hilo maana hali siyo nzuri kabisa,” alisema Mzee Majuto.

Hata hivyo, Mzee Majuto alisema kuwa, pamoja na hilo, JK amemuahidi kwamba atamnunulia trekta kwa ajili ya kulima kwenye mashamba yake ambako atapanda minazi huko Tanga ili aweze kuendesha maisha.

Source: GPL
Deo
Deo
New Member
New Member

Rais mstaafu Dr. Kikwete ajitolea kumsaidia Mzee Majuto matibabu India, pia kumnunulia trekta la kilimo Empty Re: Rais mstaafu Dr. Kikwete ajitolea kumsaidia Mzee Majuto matibabu India, pia kumnunulia trekta la kilimo

Post by Deo on Fri Apr 13, 2018 12:25 pm

pole sana king
  • Post new topic
  • Reply to topic

Similar topics

-

Current date/time is Fri May 24, 2019 10:30 pm