Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

MFAHAMU ZAIDI LELETI KHUMARO STAR WA MOVIE YA SARAFINA

CR7
CR7
Junior Member

MFAHAMU ZAIDI LELETI KHUMARO STAR WA MOVIE YA SARAFINA Empty MFAHAMU ZAIDI LELETI KHUMARO STAR WA MOVIE YA SARAFINA

Post by CR7 on Fri Apr 13, 2018 4:16 pm

LELETI KHUMALO (SARAFINA).
Muvi ya SARAFINA ni moja ya muvi au sinema maarufu sana Afrika na Dunia nzima iliyoigizwa mwaka 1992 kwa ushrikiano wa waigizaji wa marekani (Hollywood) na wale wa Afrika Kusini iliyokua na lengo la kuonesha jinsi ambavyo sera ya ubaguzi wa makaburu dhidi ya Waafrika na Wazawa wa Afrika kusini ilivyokuwa ikiendelea na ilivyokuwa ikiwaathiri watu wa Afrika ya kusini kipindi kile ililenga zaidi mauwaji ya halaiki ya WANAFUNZI wa SOWETO nchini Afrika Kusini waliokuwa wanpinga unyanyasaji wa Makaburu hao.
Kama ulishafatilia au kuangalia muvi hii utagundua kuwa Mhusika mkuu katika muvi ile alikuwa SARAFINA ambaye aliigiza kama mwanafunzi wa kike aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi wenzake kupinga ubaguzi na  uovu uliokuwa ukifanywa na viongozi wa makaburu dhidi ya wananchi weusi na wazawa  wa Afrika Kusini wakati ule.
Leo nimekuletea WASIFU wa LELETI KHUMALO maarufu kama SARAFINA ili Uweze kumkumbuka na kumfahamu vizuri
WASIFU WAKE
 
Mwonekano wake wakati akiigiza filamu ya Sarafina
LELETI KHUMALO alizaliwa 1970, ni mwigizaji wa Ki-Zulu wa Afrika Kusini aliyejipatia umaarufu  kutokana na nafasi yake ya kuongoza kama Mhusika mkuu katika filamu ya SARAFINA!, Na katika filamu nyingine kama vile HOTEL RWANDA, YESTERDAY na INVISCUS.
Leleti Khumaro alimaaarufu kama SARAFINA alizaliwa katika kitongoji cha KwaMashu , kaskazini mwa Durban, Afrika Kusini.
Leleti Khumalo (Sarafina) alionyesha nia ya kuigiza akiwa katika umri mdogo sana, Khumalo alijiunga na kundi la vijana la kuchekesha  liitwalo AMAJIKA, lililoongozwa na TU NOKWE.

Mwaka 1985 alijaribu kuimba muziki akiwa na Mtayarishaji na Mwigizaji maarufu wa Afrika Kusini MBONGENI NGEMA ambapo wimbo alioimba ulikuwa na kuwa wa kimataifa ambao ulijulikana kama  Sarafina!; NGEMA ndiye aliyeandika sehemu kubwa ya wimbo huo wa SARAFINA kwa LELETI KHUMALO. Na Mbongeni Ngema ndiye mwanaume ambaye baadae alimuoa SARAFINA.
Mwaka 1992,SARAFINA  alishirikiana sambamba na Mwana mama muigizaji kutoka Mareka aitwaye WHOOPI GOLDBERG (amabye ndiye ALIYEKUWA MWALIMU WA AKINA SARAFINA KATIKA SOMO LA HISTORIA katika muvi ile, na alijulikana kama MRS. MARY MASOMBUKA), Miriam Makeba na John kani katika filamu iliyotengenezwa chini ya kampuni ya DARELL JAMES ROOTD , FILAMU iliyoitwa ”SARAFINA!”, ambayo ilisambazwa duniani kote, na ikawa FILAMU KUBWA ZAIDI zaidi kutolewa BARANI AFRIKA. LELETI KHUMALO baadae alichaguliwa kuwania tuzo za IMAGE pamoja na waigizaji wenzake; Angela Bassett, Whoopi Goldberg na Janet Jackson.
Katika upande mwingine, mwaka 2015 LELETI alikaribishwa katika visiwa vya Zanzibar , Tanzania, kama mgeni rasmi wa sherehe maarufu FILAMU ZA KIAFRIKA ambapo waandaaji wa sherehe hiyo walikuwa wakiadhimisha miaka 18 ya shrehe hizo  zinazojulikana kama ZANZIBAR FILM FESTIVALS. Hivi sasa SARAFINA ni Muigizaji na Muongozaji wa Filamu AFRIKA KUSINI na Vipindi vya Televisheni ya Taifa Ya Afrika Kusini. (SABC)
FILAMU ALIZOIGIZA
Miongoni mwa filamu ambazo mwanamama huyu aliwahi kuigiza ni;
Rashford
Rashford
Junior Member

MFAHAMU ZAIDI LELETI KHUMARO STAR WA MOVIE YA SARAFINA Empty Re: MFAHAMU ZAIDI LELETI KHUMARO STAR WA MOVIE YA SARAFINA

Post by Rashford on Sun Apr 15, 2018 5:40 pm

movie kali sana hii haitaishaga kamwe
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 11:27 pm