Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

Julio afunguka kuondoka kwa Lwandamina

Share
avatar
CR7
Junior Member

Julio afunguka kuondoka kwa Lwandamina

Post by CR7 on Fri Apr 13, 2018 4:17 pm


Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefunguka kuwa kuondoka kwa Mzambia George Lwandamina aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, ni pigo na huenda ikawaathiri wachezaji kisaikolojia kutokana na michuano iliyopo mbele yao.

Hivi karibuni, Lwandamina aliondoka Yanga na kwenda kuingia mkataba na klabu ya nchini kwao, Zesco United ambayo alikuwa akiifundisha kabla ya kutua hapa nchini.

Julio alisema kuwa kuondoka kwa kocha huyo ni pigo kwa Yanga hasa kutokana na hali ambayo inapitia timu hiyo kwa sasa.

Julio alisema kuondoka kwa Lwandamina huenda kukawaathiri wachezaji kisaikolojia na bado wakiwa na majukumu mazito mbele yao.

“Yanga ni timu inayopambana msimu huu lakini kitendo cha Kocha Lwandamina kuondoka na timu ikiwa inamhitaji ni pigo sababu wana michuano mikubwa mbele yao.

“Lakini hawapaswi kukata tamaa sababu mimi ninamuamini (Shadrack) Nsajigwa ni kocha mzuri ambaye tayari amekaa na makocha hao wakubwa wenye uzoefu, hivyo anaweza kupambana na kuweza kuibeba Yanga,” alisema Julio.
avatar
mahunyo
Guest

Re: Julio afunguka kuondoka kwa Lwandamina

Post by mahunyo on Fri Apr 13, 2018 7:53 pm

Lwandamina ni mpuuzi tu kama wapuuzi wengine
avatar
Rashford
Junior Member

Re: Julio afunguka kuondoka kwa Lwandamina

Post by Rashford on Sun Apr 15, 2018 5:44 pm

mtu mzima anatoroka kama mtoto mjinga sana huyu kocha
avatar
CR7
Junior Member

Re: Julio afunguka kuondoka kwa Lwandamina

Post by CR7 on Sun Apr 15, 2018 5:45 pm

Re: Julio afunguka kuondoka kwa Lwandamina

Post by kichuya kona on Sun Apr 15, 2018 6:09 pm

@Rashford wrote:mtu mzima anatoroka kama mtoto mjinga sana huyu kocha
naskia amekimbia njaa
avatar
wazza
Junior Member

Re: Julio afunguka kuondoka kwa Lwandamina

Post by wazza on Thu Apr 19, 2018 5:13 pm

aende Jangwani watamuua na njaa

Sponsored content

Re: Julio afunguka kuondoka kwa Lwandamina

Post by Sponsored content


    Current date/time is Wed Dec 19, 2018 4:51 am