Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

Mzee Akilimali:" Mkwasa ni tatizo nipeni uwenyekiti niwasaidie sijaitwa Abramovich kwa bahati mbaya

Mzee Akilimali:" Mkwasa ni tatizo nipeni uwenyekiti niwasaidie sijaitwa Abramovich kwa bahati mbaya Empty Mzee Akilimali:" Mkwasa ni tatizo nipeni uwenyekiti niwasaidie sijaitwa Abramovich kwa bahati mbaya

Post by Mkweli daima on Sun Apr 15, 2018 4:26 pm

AKILIMALI:- MKWASA AMEYATAKA MWENYEWE

-Katibu wa Baraza la wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali naye ametoa neno kuondoka kwa kocha wa Yanga, George Lwandamina na kujiunga na klabu ya Zesco United.

-Asubuhi ya leo mzee akilimali amesema 
"Lwandamina ni kocha mzuri sana tukubali tu timu yangu imepoteza mtu sahihi, Yanga ilikuwa inamhitaji bado Lwandamina ila viongozi wa Yanga ndio wamesababisha yote haya"

"Katibu tumempigia kelele kila siku atangaze mchakato wa uchaguzi ili nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo ijazwe ila yupo kimya. Timu imekosa fedha za kujiendesha kwa sasa ila angekuwepo mwenyekiti angekuwa na yeye ana mawazo chanya ya kupata fedha"

"Wamevunja Katiba ya Yanga kwa matakwa yao wenyewe, matatizo ambayo yapo kwa sasa klabuni hapo yamesababishwa na viongozi waliopo kwa sasa kwa kukumbatia mambo wenyewe wamekuwa wasiri kila jambo ona sasa wanaumbuka"
Alisema Mzee Akilimali

-Mzee akilimali alipoulizwa swali yeye kama katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga inaisaidiaje klabu hiyo kwa sasa na matatizo ambayo yaliyopo mzee Akilimali alijibu 

"Katibu atangaze mchakato wa kujaza nafasi iliyoachwa na Bwana Yusuph Manji iwapo wana Yanga watataka niwe mwenyekiti wa klabu hiyo nitaisaidia kwa moyo mmoja"

"Watu hawajui jina la abramovich limetoka wapi mimi sishindwi kuisaidia klabu ya Yanga kwa sasa ila nitaisaidiaje niko nje ya mfumo" 

Alisema Akilimali kwa sauti ya upole.

Mzee Akilimali:" Mkwasa ni tatizo nipeni uwenyekiti niwasaidie sijaitwa Abramovich kwa bahati mbaya Fb_img_1523793294282-jpg Mzee Akilimali:" Mkwasa ni tatizo nipeni uwenyekiti niwasaidie sijaitwa Abramovich kwa bahati mbaya Fb_img_1523793433661-jpg

Mzee Akilimali:" Mkwasa ni tatizo nipeni uwenyekiti niwasaidie sijaitwa Abramovich kwa bahati mbaya Empty Re: Mzee Akilimali:" Mkwasa ni tatizo nipeni uwenyekiti niwasaidie sijaitwa Abramovich kwa bahati mbaya

Post by Roy on Sun Apr 15, 2018 5:57 pm

hawa wazee ndio hutuaribia timu zetu
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 11:08 pm