Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

Msuva azidi kung'ara Morocco

Msuva azidi kung'ara Morocco Empty Msuva azidi kung'ara Morocco

Post by celine dion on Mon Apr 23, 2018 11:14 am

Msuva azidi kung'ara Morocco Simon-msuva-difaa-al-jadida_1gg7tz4hh6mot15e88vyu1wki0

Winga Mtanzania anaicheza Difaa Hassan El - Jadida ya Morocco, Simon Msuva, jana amezidi kung'ara baada ya kufunga bao moja timu yake ilipocheza dhidi ya Raja Casablanca ikiwa Uwanja wake wa nyumbani.

Jadida ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-1 na katika mchezo ambao ulikuwa wa ligi kuu, na kufikisha jumla ya alama 41 na ikirejea kwenye nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi.

Bao jingine la Jadida lilitiwa kimiani na Hamid Ahadad na kuifanya timu hiyo itimize jumla ya michezo 26 msimu huu.

Msuva alijiunga na Jadida akitokea Yanga ya Tanzania, na huu ni msimu wake wa kwanza akiwa na Waarabu hao.
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 11:05 pm