Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

Historia fupi ya malkia wa nyimbo za injili Rose muhando

Historia fupi ya malkia wa nyimbo za injili Rose muhando Empty Historia fupi ya malkia wa nyimbo za injili Rose muhando

Post by david luiz on Wed Apr 11, 2018 1:15 am

Historia fupi ya malkia wa nyimbo za injili Rose muhando Rose-m10

Rose Muhando, Alizaliwa 1976 katika kijiji cha Dumila, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, Tanzania, Afrika Mashariki na ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa lugha ya Kiswahili.

Rose Muhando kabla hajawa mkristo alikuwa Muislam na ni mama wa watoto watatu. Alimpokea Yesu Kristo pale alipokuwa anaumwa na yuko kitandani akiwa na umri wa miaka 9, aliugua kwa muda wa miaka mitatu, na baadae alipona na kubadili dini na kuwa Mkristo.
Historia fupi ya malkia wa nyimbo za injili Rose muhando Rose-mhando1
Rose alianza musiziki katika kwaya iliyoko Dodoma na alikuwa mwalimu wa Kwaya katika kwaya ya Dodoma St. Mary’s katika kanisa la Kianglikana la Chimuli.

Tarehe 31/01/2005, Rose Muhando alizawadiwa tuzo ya Mtunzi mzuri wa nyimbo, Mwimbaji Bora na albamu Bora ya Mwaka. Tuzo hizo zilitolewa katika tamasha Tanzania Gospel Music Awards, 2004 Desemba 2005 alihudhuria katika tamasha la Nyimbo za Injili katika kusaidia kuchangia kwa watoto wajane dar es Salaam.

Februari 2011, Rose Muhando alisaini Mult Album Recording Deal with sony Music. Kusaini huko kulitangazwa katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Tanzania, mwezi Februari na hii ni mara ya kwanza kufanyika afrika Mashariki.

Baadhi ya albam za Rose Muhando ni,  Mteule uwe macho (2004),  Kitimutimu (2005),Jipange sawasawa (2008), Utamu wa Yesu (2012), Kamata pindo la Yesu (2015).

Tuzo alizopata 2005 Tanzania Music Awards, Best Female Vocalist & Best Religious Song(“Mteule uwe macho”)  2009 The Best Tanzanian Gospel Singer Awards: Rose Mhando;The Best Singer in Tanzania, awarded Tsh 200, 000 by Tanzania Broadcasting CorporationTBC under the Umbrella of her song called ‘Nibebe’ 2008 Kenya groove awards – best female gospel artist in Africa.
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 10:28 pm