Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.

Join the forum, it's quick and easy

Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.

Soka Sports

Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

+26
Edga
Captein Pirlo
Wire
King
depay
Kun"
Leo
human
Rashford
Mkweli daima
lallana
Roy
mikael
Deo
dUMA
moyo
kichuya kona
Chuga
lingardhinho
Dele Alli
ramsey
Hamiliton
Sandoka
Mavugo R
MO SALAH
Juma Selemba
30 posters

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Juma Selemba
    Juma Selemba
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Juma Selemba Tue Apr 10, 2018 10:49 am

    Wanajukwaa wa  soka sport habarini za muda Huu? natumai mu wazima wa afya  hii ni mada maalum kwa wadau wa soka na TFF,
    Tanzania tumekuwa nyuma sana kimpira kwanzia ngazi ya vilabu mpaka timu ya Taifa, Tumezidiwa mpaka na majirani zetu wanaotuzunguka,
    Mimi nafikiri kuna tatizo mahali flani ambalo linahitaji ufumbuzi,

    sisi kama mashabiki tumejitahidi sana kuzipa support timu zetu lakini inafika mahala tunakatishwa tamaa kabisa hususa ni timu ya taifa imekuwa haifanyi vizuri kwa muda murefu sana,

    Je, wewe kama mdau wa soka unatoa ushauri kipi kifanyike au turekebishe wapi ili tuweze kupiga hatua?

    NAWASILISHA.
    MO SALAH
    MO SALAH
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by MO SALAH Tue Apr 10, 2018 10:57 am

    Kwa upande wangu naona sisi bado hatujawekeza katika soka, isipokuwa tunataka tu kucheza soka,
    Hebu tusitake mafanikio ya haraka haraka kabla hatujatengeneza njia za mafanikio, Kwanza tuwekeze katika vijana,
    Vijana wadogo ndio kizazi kijacho cha soka hebu tazama timu za ulaya karibu kila timu ina academy na academy zao zinazingatiwa kwa asilikmia mia moja,

    Mfano mzuri tazama kikosi cha Taifa staz ni kilekile tu kila mwaka, Hata mechi za kirafiki makocha hawataki kuweka vijana wapya ili wakomae,
    tazama serengeti boys wanavyotelekezwa baada ya michuano yao kumalizika,

    cha msingi tuwekeze kwanzia chini kabisa kwenye shina

    AHSANTE
    Mavugo R
    Mavugo R
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Mavugo R Tue Apr 10, 2018 11:30 am

    Rushwa na kujuana vikipigwa marufuku tutasonga mbele
    Sandoka
    Sandoka
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Sandoka Tue Apr 10, 2018 12:28 pm

    Mfumo wa TFF umetawaliwa na figisu figisu, watu wanaojua mpira wanawekewa vikwazo kugombea nafasi za juu,

    kiupande wangu mimi naona TFF ndio kuna tatizo kubwa TFF tunaomba mjitazame upya
    Hamiliton
    Hamiliton
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Hamiliton Tue Apr 10, 2018 6:07 pm

    Tuwaache makocha wawe mameneja
    tanzania kumekuwa na kasumba ya kocha kuingiliwa majukumu yake imefika mpaka hatua wachezaji wanasajiliwa tu pasipo matakwa ya kocha,
    kwa mtazamo wangu naona bora tuwaache makocha wfanye ujuzi wao bila kuingiliwa, Tazama ulaya kocha ndiye manager wa timu.
    Lakini tanzania makocha wanapelekeshwa na viongozi wa timu mpaka kufikia hatua ya kupangiwa kikosi hii sio sawa kabisa
    ramsey
    ramsey
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by ramsey Wed Apr 11, 2018 1:36 am

    Tabia ya kuleta makocha wakigeni yaelekea siyo muarobaini wa kutufanya tutambe kwenye viwanja vya soka duniani lakini hatua hizi zaweza kutusoge za mbele ya hapa tulipo:-

    a) Kutambua ya kuwa vilabu ndiyo msingi wa maendeleo ya soka usiwe na wa domo tu bali uanze na kutoa ruzuku kwa vilabu kutoka serikalini ili vitoe chachu ya mchezo huu. Aidha vilabu vimekuwa vikiendesha kazi zake kutokana na ridhaa ya wafadhili ambao wengi wao huja na malengo yao binafsi ambayo siyo lazima yaoane na mahitaji ya vilabu husika. Ruzuku hizi zitapunguza au kuondoa kabisa tegemezi za vilabu kutoka kwa wafadhili ambao hutoa mchango mkubwa wa kudumaza soka letu badala ya kuliendeleza.

    Kwa kuanzia vilabu vya darajala premier, kila kilabu kipewe shilingi bilioni moja kila mwaka na daraja la kwanza shilingi milioni mia mbili hamsini kila mwaka kwa kila kilabu. Daraja la pili shilingi milioni mia kwa mwaka kwa kila kilabu. Daraja la tatu shilingi milioni hamsini kwa kila kilabu na kwa mwaka. Masharti ya kuendelea kuzipata fedha hizi ni kuwa kila timu itabidi kupeleka hesabu zao zilizokaguliwa kwa CAG kila mwaka kuhakikisha fedha hizo zimetumika vyema kwa malengo yaliyokusudiwa......

    b) Wachezaji wa timu ya taifa kulipwa mshahara wa kila mwezi kama nchi nyinginezo duniani. Mfano, Afrika ya Kusini mchezaji hulipwa dola za kimarekani elfu nne kila mwezi. Hii itawaongezea wachezaji wa Taifa Stars ari ya kuichezea timu ya taifa badala ya mfumo uliopo hivi sasa.

    Kwa kuanza kila mchezaji alipwe mshahara wa dola 2,000 kwa mwezi mbali ya posho wakati wa mazoezi au mechi au mshahra wake wa kilabuni kwake atokako.........
    ramsey
    ramsey
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by ramsey Wed Apr 11, 2018 1:37 am

    Makosa yapo sehemu kibao, na mengine yanatokana na kutaka sifa bila ya kufanya chochote cha maana. TFF imeshindwa kabisa kulinda timu za mikoani mpaka tunajikuta tuna ligi dhaifu na isiyokuwa na ushindani.

    Kanuni za usajili wa wachezaji zinaumiza sana vilabu vidogo kiasi kwamba wachezaji wa timu ndogo wanachukuliwa kirahisi mno na timu kubwa na kusababisha timu hizi kuwa na utitiri wa wachezaji wa mazoezi zaidi kuliko wa kucheza mechi.

    Ligi yetu haieleweki kama ni ya kulipwa au ya ridhaa,maana kuna timu ambazo zinaendeshwa ktk mfumo wa kiprofessional lakini zinacheza ligi ya ridhaa,hapo unakuta chances za kumfanya mchezaji kuwa endelevu ni kidogo mno kwa vile anasajiliwa kiprofessional,anacheza rihaa na mkataba unakuwa feki kwa vile mchezaji mwenewe anakuwa hana uhakika wa tiba nzuri akiumia kwa vile hata bima yake ni ya kimtindomtindo tu.
    Dele Alli
    Dele Alli
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Dele Alli Wed Apr 11, 2018 1:42 am

    “Ukiangalia kwa juu utaanza kuulaumu uongozi wa TFF na mambo mengine mengi ila tatizo kuu lipo katika klabu kwani hawajui kuwa kupitia wawo tunaweza kuwa na vipaji lukuki na kuendeleza soka la nchi hii.
    lingardhinho
    lingardhinho
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by lingardhinho Wed Apr 11, 2018 1:57 am

    changamoto kubwa ni wachezaji wenyewe kushindwa kujituma pamoja na kuwa na elimu ndogo ya soka.
    Chuga
    Chuga
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Chuga Wed Apr 11, 2018 3:11 am

    MOJA ya vitu vinavyochangia ligi yoyote ya soka ulimwenguni ifanikiwe, ni pamoja na kuwa na mpangilio mzuri kwa maana ya ratiba. Ratiba lazima izingatie matakwa ya wadau wake.
    Kwa mtindo huo hakutakuwa na lawama na hata kama kutatokea mabadiliko, hayatalalamikiwa kwa kiasi kikubwa endapo wadau wanashirikishwa katika kila hatua na si vinginevyo.
    Uendeshwaji wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, umekuwa ukigubikwa na vimbwanga vya hapa na pale, kubwa likiwa ni lile la kubadili ratiba kila mara kana kwamba wahusika wa kutengeneza ratiba hiyo hawakujua kuwa kuna baadhi ya matukio lazima yapewe nafasi katikati ligi hiyo.
    kichuya kona
    kichuya kona
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by kichuya kona Thu Apr 12, 2018 11:53 am

    Taifa Stars wakamuombe radhi mzee Mwinyi..
    moyo
    moyo
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by moyo Thu Apr 12, 2018 12:50 pm

    tatizo huanzia shinani TFF bado ni tatizo kubwa, Tff imejaa wanachama nguli wa klabu za soka, ratiba zinapangwa kwa upendeleo na hujuma kwa hali kama hii soka halitaendelea kamwe
    Anonymous
    THABITHA
    Guest

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by THABITHA Thu Apr 12, 2018 1:53 pm

    kimtazamo wangu mimi, naona mpira ni pesa
    kwa mfano ngazi ya vilabu huwezi kufanya vizuri wakati timu yako inasua sua kiuchumi

    hebu tazama mpira wa nje uko juu sababu ya pesa,

    huu ni wakati vilabu vyetu viamue rasmi kufanya uwekezaji ktk soka,
    wajenge viwanja bora, wachezaji walipwe vizuri n.k hapo ndipo soka la Tz litainuka
    dUMA
    dUMA
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by dUMA Thu Apr 12, 2018 8:22 pm

    shule nayo inachangia kichwani
    Deo
    Deo
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Deo Fri Apr 13, 2018 12:29 pm

    kichuya kona wrote:Taifa Stars wakamuombe radhi mzee Mwinyi..

    mwinyi alishatengua kauli mbona
    mikael
    mikael
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by mikael Fri Apr 13, 2018 6:44 pm

    tuache maneno maneno tucheze soka, watanzania tumekua na kasumba ya mpira kuuchezea midomoni
    mikael
    mikael
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by mikael Fri Apr 13, 2018 6:45 pm

    tuache maneno maneno tucheze soka, watanzania tumekua na kasumba ya mpira kuuchezea midomoni
    Roy
    Roy
    Founder

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Roy Fri Apr 13, 2018 8:07 pm

    mikael wrote:tuache maneno maneno tucheze soka, watanzania tumekua na kasumba ya mpira kuuchezea midomoni

    kweli kabisa broo soka la tanzania ni mdomoni
    lallana
    lallana
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by lallana Fri Apr 13, 2018 8:36 pm

    mimi nafikiri ingewekwa sheria timu kama haina uwanja wa maana na pesa z kujiendesha hakuna kuingia ligi kuu
    lallana
    lallana
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by lallana Fri Apr 13, 2018 8:37 pm

    kichuya kona wrote:Taifa Stars wakamuombe radhi mzee Mwinyi..

    kwa kosa lipa?
    Mkweli daima
    Mkweli daima
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Mkweli daima Sun Apr 15, 2018 4:30 pm

    kwanza watanzania wenyewe tuanze kusapot timu zetu, haiwezekani ynasema mpira ni pesa wakati timu yako hutaki kuichangia mapato angalau hata kununua jezi tu, je, unategemea hiyo pesa wataitoia wapi?
    pili viwanjani mashabiki hawajai mpaka iwe ni mechi ya simba na yanga je, hayo mapato unategemea timu itapata lini?

    ulaya hata mechi za kawaida mashabiki wanajaa sana na jezi wananunua sana ndio maana timu zao zinahela nyingi
    Mkweli daima
    Mkweli daima
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Mkweli daima Sun Apr 15, 2018 4:32 pm

    dUMA wrote:shule nayo inachangia kichwani

    hahaha kweli hilo nalo pia wachezaji wetu wengi shule hamna ndio maana mara kwa mara hutokea migogoro ya mikataba na timu zao while ulaya hicho kitu hatujawai kukisikia
    Rashford
    Rashford
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Rashford Sun Apr 15, 2018 5:38 pm

    Tatizo bongo usimba na uyanga sana
    kichuya kona
    kichuya kona
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by kichuya kona Sun Apr 15, 2018 6:06 pm

    kwa kosa lipa?
     kosa lipi?
    human
    human
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by human Sun Apr 15, 2018 9:23 pm

    Tatizo Mpira unaingiliwa na siasa

    ushauri kwa TFF watafute suluhisho kwa kusikiliza maoni ya wadau mbalimbali,

    waache kujifanya wao wanajua kila kitu
    Leo
    Leo
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Leo Tue Apr 17, 2018 11:49 am

    Mpira wa Tanzania ili uendelee inabidi tuache kuendekeza maswala ya akina akilimali na akina kilomoni, Timu tuzibinafsishe kwa wawekezaji.
    maswala ya timu kumilikiwa na wananchi, hapo hapo serikali ina hisa hapo hapo mwekezaji anahisa haya ndio yanatukwamisha,
    matokeo yake kwenye maamuzi kila mtu anasema lake
    Leo
    Leo
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Leo Tue Apr 17, 2018 11:56 am

    Mkweli daima wrote:kwanza watanzania wenyewe tuanze kusapot timu zetu, haiwezekani ynasema mpira ni pesa wakati timu yako hutaki kuichangia mapato angalau hata kununua jezi tu, je, unategemea hiyo pesa wataitoia wapi?
    pili viwanjani mashabiki hawajai mpaka iwe ni mechi ya simba na yanga je, hayo mapato unategemea timu itapata lini?

    ulaya hata mechi za kawaida mashabiki wanajaa sana na jezi wananunua sana ndio maana timu zao zinahela nyingi
    ni kweli kabisa watanzania hatuna hamasa ya kuongezea timu zetu kipato, tazama nchi za wenzetu kama uingereza wanaisapot timu kwa kununua jezi, bendera, mitandio,picha n.k
    pia viwanjani wanajaa kila mechi unategemea kwanini timu isiwe na pesa kwa mfano?
    Kun
    Kun"
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Kun" Thu Apr 19, 2018 12:39 pm

    .

    Last edited by Kun" on Thu Apr 19, 2018 12:41 pm; edited 1 time in total
    Kun
    Kun"
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Kun" Thu Apr 19, 2018 12:40 pm

    Soka la bongo likipata rasilimali (fedha, viongozi wenye utashi, vipaji, mashabiki na wapenzi) nyingi zaidi linaweza kuendelea mfano mzuri ni Azam sababu wana uwezo wa kifedha na utashi wamefika hapo walipo wana 4 yrs lkn wana uwanja, timu za vijana, wamekuwa 1 runner up ktk kila mashindano waliyoshiriki msimu uliopita wa ligi kwa hyo kwa mfano wa azam ni wazi kuwa mafanikio katika soka la bongo yanawezekana.

    Tukija upande mwingine soka letu liko kimizengwemizengwe sana hata professionalism inashindikana u-Simba na u-Yanga uko sana kuanzia TFF, marefa, waandishi viongozi wa serikali wote wana usimba au uyanga na still timu hizi 2 kubwa bado nazo zinaongozwa kiujanjaujanja hawana mission wala vision. 

    Athari za u-Simba na u-Yanga hizi timu zimekuwa zikipendelewa sana na marefa na TFF mfano ni lile zengwe alilopigwa Moro Utd ile iliyokuwa inafadhiliwa na Balabou. 

    Hata mashabiki mikoani wamekuwa wakisaliti timu zao pindi zinapocheza na hizo timu. 

    Mimi ni mdau wa timu ya AFC Arusha, kuna kipindi tulikuwa tunacheza ligi kuu na tulikuwa ktk ukata mgumu na msaada umetafutwa haukupatikana then Yanga walikuja washabiki walichanga laki 3 on the spot kwa Yanga ambayo tayari ina wadhamini na vitega uchumi huku wakijua timu yao ya nyumbani ni fukara.... 

    Kwa upande wangu; ili soka letu liendelee kabla ya kuwekeza fedha na vitu vingine tuondoe usimba na uyanga sawa ni vilabu vikubwa na vitabakia kuwa hivyo ila unazi upungue ili kutoa fare playground kwa wote
    depay
    depay
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by depay Thu Apr 19, 2018 1:06 pm

    Kwa upande wa soka la Bongo, hadi makocha na wadhamini wengine wana unazi wa u-simba na u-Yanga. Unakuta timu haina sababu ya kupoteza mchezo unakuta kiongozi wao anawashawishi wachezaji wapoteze mchezo ili tu Simba au Yanga iwe mbali.

    Kwa kusema makocha wazalendo walipwe mamilioni ya shilingi ndio tufike mbali hakuna kitu kama hicho! Tutafika mbali kama uongozi mzima wa soka Tz utabadilika na kufuata misingi ya maendeleo. Mfano; African Lyon toka mwaka jana wamepata udhamini lakini TFF wanaukatalia udhamini huo halafu wanajifanya wanataka soka likue.

    Kuendelea kwa soka Bongo ni pindi pale unazi wa kishamba utakapoisha..

    Ahsanteni.
    King
    King
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by King Thu Apr 19, 2018 1:17 pm

    uwezo wa soka tunao watanzania lakini tatizo kubwa lipo kwa viongozi mpango wa kupangua kikosi cha timu ya taifa mara kwa mara hilo ni tatizo,viongozi kuweni makini ili taifa letu liendelee kisoka.
    Wire
    Wire
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Wire Thu Apr 19, 2018 4:03 pm

    lallana wrote:mimi nafikiri ingewekwa sheria timu kama haina uwanja wa maana na pesa z kujiendesha hakuna kuingia ligi kuu

    wakifanya hivyo basi zitaingia timu zisizozidi tano
    Captein Pirlo
    Captein Pirlo
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Captein Pirlo Thu Apr 19, 2018 4:09 pm

    Tukitaka soka iwe na nguvu na tusonge mbele lazima japo ni ngumu sana ni muhimu sana kama simba na yanga zinaweza kufa au kusambaratika Maana ni chanzo cha fitina za mpira!
    Edga
    Edga
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Edga Thu Apr 19, 2018 4:20 pm

    Huku kwetu Tanzania mpira unachezwa zaidi na viongozi , ndani ya uwanja , nje ya uwanja na mahakamani , kwetu kununua mechi ni jambo la kawaida sana ! Waamuzi kununuliwa siyo siri tena .

    Soka la Tanzania limedumaa mithili ya MTOTO ALIYEBEMENDWA ! hivi ninavyoandika haya viongozi wa TFF wako mahakamani kwa sababu zinazofahamika kama FITNA ZA UCHAGUZI ! Yaani viongozi wa soka wanapangwa kutoka nje ya soka lenyewe , aibu sana !
    Zizzou
    Zizzou
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Zizzou Thu Apr 19, 2018 4:30 pm

    TZ mpira ulikufa toka miaka ya 1970 kilichobaki ni ubishi na mazoea tu. We umeona wapi mtu kama Mze Akilimali asiye na mchango wowote ndani ya timu eti anaogopewa na kama abugiii ugoro basi timu haiendi kucheza.
    Justine Jr
    Justine Jr
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Justine Jr Thu Apr 19, 2018 4:43 pm

    Mambo soka sisi hatuyawezi ni bora tuangalie mambo ya msingi ya kimaendeleo katika nchi yetu.
    Virgin Jack
    Virgin Jack
    New Member
    New Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Virgin Jack Thu Apr 19, 2018 4:57 pm

    Justine Jr wrote:Mambo soka sisi hatuyawezi ni bora tuangalie mambo ya msingi ya kimaendeleo katika nchi yetu.
    mh napita Very Happy Very Happy Very Happy
    wazza
    wazza
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by wazza Thu Apr 19, 2018 5:14 pm

    Chuki za uchaguzi na hila vimefanya mpaka malinzi leo hii yuko Lumande, sasa tujiulize kama tu uchaguzi wa TFF unatawaliwa na visasi vya namna hii hivi hapo kuna mpira kweli au upuuzi?
    wazza
    wazza
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by wazza Thu Apr 19, 2018 5:16 pm

    Virgin Jack wrote:mh napita Very Happy Very Happy Very Happy

    Kwaheli! Arrow
    wazza
    wazza
    Junior Member

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by wazza Thu Apr 19, 2018 5:22 pm

    dUMA wrote:shule nayo inachangia kichwani

    Shule kwa nani Very Happy Very Happy Very Happy unamaanisha wacheza soka wetu hawana shule kichwani?

    Sponsored content

    Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania? Empty Re: Uzi maalumu wa kutoa maoni au ushauri, Nini Tufanye ili kuboresha soka letu la Tanzania?

    Post by Sponsored content

      Current date/time is Sun May 12, 2024 6:37 pm