Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.

Join the forum, it's quick and easy

Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.

Soka Sports

Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

    JUPP HEYNCKES NA KIUNGO CHA SIRI.

    joker
    joker
    New Member
    New Member


    JUPP HEYNCKES NA KIUNGO CHA SIRI. Empty JUPP HEYNCKES NA KIUNGO CHA SIRI.

    Post by joker Tue Apr 10, 2018 12:34 pm

    JUPP HEYNCKES NA KIUNGO CHA SIRI. 30571310

    Jumamosi iliopita klabu ya FC Bayern München ilitwaa ubingwa wake wa saba mfululizo nchini Ujerumani tena kwa tofauti ya alama 20 dhidi ya mtu anaeshika nafasi ya pili. Lakini kocha wao Jupp Heynckes ana siri na hii timu, siri ambayo umma hauijui. Bayern Munich haijawahi kupata tabu ikiwa na huyu jamaa. Ameifanya ile klabu iishi kama mtoto mdogo asiye na dhambi.

    Huyu mzee anaijua Bayern Munich kuliko unavyofikiria. Alipewa timu kwa mara ya kwanza mwaka 1987 mpaka 1991 akaipa timu mataji 2 ya Bundesliga. Baada ya miaka 21 timu akaichukua tena na msimu wake wa mwisho anatangaza kustaafu akawaacha the Bavarians na mataji 3 yani Bundesliga, DFB-Pokal na Klabu bingwa Ulaya.

    Huyu mzee nikukumbushe hakufukuzwa bali alistaafu mwenyewe ukufunzi. Unadhani kuna namna Bayern walitaka kuondokewa na mtu kama huyu? Hapana na ndio maana haraka sana walishuka chini na kumuomba huyu mzee arudi. Hata United naamini wanatamani wamrudishe Sir Alex Ferguson kwenye timu wakiamini huyu mtu anaijua timu kuliko mtu mwengine yoyote tena bila hata kuangalia aina gani ya wachezaji alionao.

    Mwanzoni mwa msimu Bayern ilionekana kuwa na mwanzo mgumu wa maisha mbele ya Borussia Dortmund lakini tangu Heynckes airudie timu yake hiyo sio hali halisi tena. Bayern wametwaa Bundesliga na wako mbioni kufanya mengine makubwa. Bayern walimmisi sana huyu jamaa na kiukweli watu kama hawa ni wachache sana kwenye soka.

    Unaweza ukahisi Bayern wanawekeza kwenye mafanikio yao na ni klabu kubwa lakini wapo makocha ambao wamewahi kufanya vizuri kwenye vilabu kwa mara ya kwanza lakini mara ya pili baada ya kurudi wakashindwa. Mfano ni Jose Mourinho ndani ya Chelsea. Alifanya vizuri kwenye spell yake ya kwanza lakini baada ya kurudi kwa mara ya pili akafanya vizuri msimu wa kwanza lakini msimu wa pili tena akiwa na wachezaji walewale alikuwa anapigana kutoshuka daraja.

    Hebu fikiria Heynckes ameifundisha Bayern mara 3 tena kwa miaka ilioachana. Mara ya kwanza ikapita miaka 21 akaondoka na kurudi baada ya miaka mingine 4 akiwa na kundi la wachezaji tofauti lakini bado amepata mafanikio. Hapa utagundua kuwa Heynckes ana kitu cha ziada ukiachana tu na mbinu na uwekezaji wa Bayern ana kitu cha ziada ambacho umma haukujui na kimemsaidia kufanikiwa kwenye klabu moja kwa nyakati tofauti tena zilizoachana.

    Mabadiliko kwake yeye ni kama hakuna mabadiliko. Amewashinda wapinzani wake wakubwa ambao walikuwepo kwenye ligi na kuizoea vizuri lakini yeye amerudi na ni kana kwamba alikuwepo tu muda wote huo.

    Yani mtu anaipa timu mafanikio bila ya kujali ana kina nani kama wachezaji kwenye akiba yake. Mimi huwa nasema huyu ana mahusiano na timu na sio wachezaji. Miaka 21 ni kipindi ambacho mtu anaweza asimkumbuke mwanae aliepoteana nae lakini jamaa hajawahi kukishau kiungo cha siri ambacho kimekuwa kikimfanya kila akiwepo Bayern Munich afanikiwe.

      Current date/time is Fri May 17, 2024 11:11 am