Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.

Join the forum, it's quick and easy

Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.

Soka Sports

Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

    Mziki Wa Bongo Fleva Unakufa Kwasababu Ya Wasanii Kupenda Kiki- Ney Wa Mitego

    Nahumu
    Nahumu
    New Member
    New Member


    Mziki Wa Bongo Fleva Unakufa Kwasababu Ya Wasanii Kupenda Kiki- Ney Wa Mitego Empty Mziki Wa Bongo Fleva Unakufa Kwasababu Ya Wasanii Kupenda Kiki- Ney Wa Mitego

    Post by Nahumu Tue Apr 10, 2018 1:12 pm

    Mwanamuziki wa Bongo fleva, Ney Wa Mitego amefunguka na kuamua kuwachana wanamuziki wenzake wote anaodai kuwa wanapenda kutafuta kiki kuliko kufanya mziki unaoeleweka.

    Ney Wa Mitego alitumia mtandao wa kijamii kufikisha ujumbe wake ambao alidai wasanii wa bongo fleva kupenda kutafuta kiki kunapelekea kuua mziki kwani kiki inakuwa kubwa na mziki unakuwa wa kiwango cha chini sana kupita promo uliopata.

    Ney Wa Mitego alifunguka:

    Wasanii wenzangu kusema kweli kuna kitu nakiona kwenye gemu yetu, kwenye mziki wetu wa bongo fleva tuna kibarua kikubwa cha kurudisha mziki kwenye mstari ulionyooka kwa sababu imefika time watu sasa hivi wanatengeneza kiki kubwa alafu mziki mdogo, yaani kiki zimekuwa mbele mziki uko nyuma unasindikiza, tukiendelea hivi miaka miwili mitatu ijayo naiona bongo fleva ikiwa imepotea kama bongo movie ambavyo imepotea, Kama tusipokuwa makini kuamua kufanya kazi na mini viwe ni vitu vya kusindikiza mziki, sahivi mambo yamebadilika imefika time watu wanatengeneza kiki ambazo yaani hazielezeki alafu mziki unachukua nafasi ndogo sana unasindikiza kiki jamanii ehee tunajisahau tuamke turudishe mziki wetu kwa sababu tunakuwa tunawalemaza sana mashabiki zetu”.

    Wasanii wengi wa Bongo fleva siku hizi wamekuwa na kawaida ya kutengeneza kitu kinachoitwa kiki yaani wanajitengenezea skendo kubwa kwenye mitandao ya kijamii mara tu pale wanapokaribia kutoa nyimbo mpya ili tu wawe wanazungumziwa kipindi nyimbo inatoka kwa madai kazi inapata promo kubwa na ushabiki mkubwa.

    nini maoni yako?:

      Current date/time is Sun May 19, 2024 8:19 am