Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

EFA yatangaza mabadiliko kadhaa katika Michuano ya Klabu Bingwa na EUROPA kuanzia msimu ujao

EFA yatangaza mabadiliko kadhaa katika Michuano ya Klabu Bingwa na EUROPA kuanzia msimu ujao Empty EFA yatangaza mabadiliko kadhaa katika Michuano ya Klabu Bingwa na EUROPA kuanzia msimu ujao

Post by david luiz on Wed Apr 11, 2018 1:13 am

Shirikisho la soka barani Ulaya(UEFA) limethibitisha kwamba timu za soka zinaweza kuweka majina 12 ya wachezaji wa ziada kwenye mechi za fainali za Ligi ya Mabigwa(UEFA Champions), Ligi ya EUROPA na Super Cup. Kwa sasa idadi hiyo ni wachezaji 7
EFA yatangaza mabadiliko kadhaa katika Michuano ya Klabu Bingwa na EUROPA kuanzia msimu ujao Uefa-jpg
Aidha, katika sheria hiyo mpya ambayo itaanza kutumia msimu ujao wa soka, timu zitaweza kufanya mabadiliko mara nne katika hatua ya mtoano ya michuano, huku badiliko hilo la nne likiruhusiwa wakati wa dakika za nyongeza

Timu zitaruhusiwa kusajili wachezaji wapya watatu kwenye michuano hiyo baada ya hatua ya makundi kumalizika. Ikimaanisha mchezaji anaweza kuchezea timu moja wakati wa hatua ya makundi halafu akasajili na timu nyingine(kwenye dirisha la usajili) na timu hiyo kumsajili UEFA kucheza katika hatua ya mtoano

Pia katika UEFA mechi zake zote zitakuwa zinachezwa muda wa 8pm GMT (kwa Tanzania: saa 4:00 usiku majira ya joto, saa 5:00 usiku majira ya baridi)

Katika michuano ya michuano ya EUROPA hatua ya makundi mpaka 16 bora mechi zitakuwa zinaanza saa 5:55pm GMT na 8pm GMT(Kwa Tanzania; 1:55 usiku na 4:00 usiku majira ya joto, 2:55 na 5:00 majira ya baridi). Michezo ya robo, nusu na fainali itachezwa saa 8pm GMT (kwa Tanzania: saa 4:00 usiku majira ya joto, saa 5:00 usiku majira ya baridi)

    Current date/time is Mon Jul 22, 2019 7:17 pm