Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.

Join the forum, it's quick and easy

Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.

Soka Sports

Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

    Hivi huyu ‘Boccogoals’ ni ‘jogoo la shamba’, au ‘mfalme’ wa ugenini?

    Roy
    Roy
    Founder


    Hivi huyu ‘Boccogoals’ ni ‘jogoo la shamba’, au ‘mfalme’ wa ugenini? Empty Hivi huyu ‘Boccogoals’ ni ‘jogoo la shamba’, au ‘mfalme’ wa ugenini?

    Post by Roy Fri Apr 06, 2018 1:48 pm

    Hivi huyu ‘Boccogoals’ ni ‘jogoo la shamba’, au ‘mfalme’ wa ugenini? Img-2010

    NAHODHA wa Simba SC, John Bocco alifunga magoli yote mawili ya timu yake katika ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Njombe Mji FC siku ya Jumanne hii na kuisaidia timu yake kuongeza ‘gap’ la pointi-kutoka alama pacha 46 hadi pointi tatu zaidi dhidi ya wanaoshika nafasi ya pili-mabingwa watetezi Yanga SC.

    Baada ya kuamua michezo migumu Tanzania Prisons 0-1 Simba, Ndanda FC 0-2 Simba, Kagera Sugar FC 0-2 Simba, Bocco amefanya hivyo kwa mara nyingine katika uwanja wa Sabasaba, Njombe. Bila shaka huyu ni ‘mfalme’ wa viwanja vya ugenini msimu huu. Wakati huu timu ikionekana kuwa na wachezaji kadhaa bora kama Okwi, Erasto Nyoni, James Kotei, Shiza Kichuya hata Jonas Mkude, Said Ndemla , Asante Kwasi na Shomari Kapombe, upande wangu Bocco ndiye mchezaji muhimu zaidi.

    Katika uwanja wa Sokoine Novemba mwaka jana wakati ikidhaniwa mchezo kati ya Prisons na Simba ungemalizika kwa suluhu, Bocco akafunga kwa juhudi binafsi mbele ya walinzi wa Prisons zikiwa zimesalia dakika chache mchezo kumalizika. Simba ikashinda kwa mara ya kwanza dhidi ya mabingwa hao wa zamani wa Tanzania katika misimu mitano iliyopita. Amekuwa akiibuka nyakati muhimu mchezoni na kumaliza mechi.

    Haitoshi, Bocco akaenda kufunga magoli yote mawili katika uwanja wa Nangwanda wakati ambao timu ilikuwa imetoka kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi-kumuondoa Joseph Omog na kumpa kibarua kocha msaidizi Masoud Djuma. Bocco akafunga goli la uongozi katika uwanja wa Kaitaba wakati mechi ikionekana itamalizika bila magoli mwezi Januari-mwezi ambao pia alitwaa tuzo binafsi ya mchezaji bora wa mwezi VPL.

    Nahodha huyo wa zamani wa Azam FC alifunga pia katika sare ya Mwadui FC 2-2 Simba Mwezi uliopita katika uwanja wa Kambarage, na Jumanne hii amefikisha magoli saba katika michezo mitano ambayo Simba wamecheza nje ya Dar es Salaam. Wakati Mganda, Emmanuel Okwi akionekana ni ‘mfalme’ katika viwanja wa Uhuru na Taifa (Dar,) Bocco ni mfungaji ambaye Simba ilimkosa tangu alipoondoka Mzambia, Felix Sunzu , Mrundi, Amis Tambwe na Mganda, Hamis Kiiza.

    Amefunga jumla ya magoli 12 katika VPL msimu huu, saba akifunga katika viwanja ambavyo ni nadra sana kwa Simba kupata ushindi. Simba imekuwa ikihangaika kurudisha ubingwa wa ligi kuu tangu walipoupoteza msimu wa 2011/12 na bado wanakabiliwa na mtihani mkubwa msimu huu kwa maana wanapaswa walau kushinda michezo nane kati ya tisa iliyosalia ili washinde ubingwa. Si rahisi na kama hili halitotokea kwa mara nyingine itakuwa pigo kubwa zaidi maana wana mfungaji ambaye anaweza kuwapa matokeo katika viwanja ambavyo walikuwa wakishindwa kufanya hivyo, Bocco.

    Huyu Bocco amewasahaulisha watu kuhusu Laudit Mavugo ambaye katika msimu wake huu wa pili ameifungia Simba jumla ya magoli tisa (sita msimu uliopita na matatu msimu huu.) Bocco ni mchezaji ambaye kujituma kwake hasa baada ya baadhi ya watu (miongoni mwao mimi) kuuponda usajili wake kumemfanya awe bora zaidi.

    Kuwa kwake bora kumeifanya timu kuendelea kunyanyuka na kuwa na uhakika wa kupata magoli ya kutosha kwa kuwa wana wafungaji wawili wa uhakika huku Kichuya akiwa kama nyongeza nyingine yenye ubora. Sikuanza kumkubali, Bocco hivi sasa, ni mchezaji ambaye nilikuwa nikisisitiza ni bora tangu mwaka 2011 na niliishia kupondwa tu na wanazi wa Simba na Yanga SC.

    Huyu ni mfungaji bora wa VPL miaka saba iliyopita tena angali kinda. Ndio maana niliukosoa mno uongozi wa Azam FC ulivyokubali kumuacha huru mshindi huyo wa VPL 2013/14, Kagame Cup 2015 na mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 na kupanda VPL mwaka mmoja baadae.

    Hivyo, nieleweke kuwa nilipinga usajili wake Simba kwa kuamini halikuwa chaguo sahihi lakini sasa amekuwa tofauti na matarajio na hata wale niliokuwa nikiwaambia misimu ya nyuma kuwa Bocco ni mfungaji mahiri na kunipinga sasa wanamshangilia.

    Kama Simba itafanikiwa kutwaa taji msimu huu itakuwa ni mafanikio makubwa sana kwao, lakini watakuwa wanapaswa ‘kimoyo moyo’ kusema ‘Asante Bocco’ japo wanapaswa kumpongeza sana kwa jitihada zake binafsi uwanjani. Bocco anajituma mno, anajitolea sana na magoli yake yanajielezea namna mchezaji anavyoweza kubadilisha ‘uelekeo wa mawazo ya wafuatiliaji’ wengi wa mchezo wake.

    Huyu Bocco sijui ni ‘nabii asiyekubalika kwao?’ Maana hata timu ambayo aliifungia magoli likiwemo lile muhimu zaidi lililoipandisha daraja Azam FC miaka kumi iliyopita, timu ambayo aliifungia goli lililowapa taji la kwanza la VPL na pekee hadi sasa, timu ambayo aliifungia goli lililowapa taji la kwanza la Kimataifa-Kagame Cup ilimkataa.

    Ama huyu ‘Boccogoals’ ni ‘jogoo la shamba lisilowika mjini’ maana hawa wanaomshangilia sasa nao walikuwa wakimpinga mno kiasi cha kufanya astaafu kuichezea Taifa Stars akiwa na miaka 23 mwaka 2012 wakati huo akizinyanyasa Simba na Yanga vile alivyokata. Ila, hakuwahi kuheshimiwa kama anavyoheshimiwa sasa.

    Huyu ni mchezaji pekee wa Kitanzania kuifunga Simba ‘Hat trick’-sina kumbukumbu na mwingine, ndiye mfungaji aliyezifunga Simba na Yanga mara nyingi zaidi tangu kuanzishwa kwa vilabu hivyo, lakini alipingwa vikali. Leo hii akiwa anachezea uzoefu na kujituma ndani ya Simba ndio anaonekana bora?

    Nakuwekea kumbukumbu hi ya mahojiano ambayo nilipata kufanya na Bocco mwaka 2011-number10 magazine

    Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) John Bocco, ni mmoja ya washambuliaji ambaye mashabiki wengi wa soka nchini ‘hawamkubali’ kivile kutokana na aina ya mchezo wake wa taratibu.

    Lakini pamoja na mtazamo wa mashabiki, hali ni tofauti anapokuwa katika klabu yake ya Azam FC, kwani ni moja ya wachezaji kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo. Bocco amekuwa akifunga magoli muhimu kwa timu yake hata dhidi ya timu za Simba na Yanga.

    Swali: Mshambuliaji gani unadhani ni bora zaidi kuwahi kucheza naye timu moja?

    Bocco: Washambuliaji wote niliopata kucheza nao niliwaona wazuri, sijajua ni kwa sababu ya ‘type’ yangu ya uchezaji kwa sababu nimecheza na washambuliaji wengi wenye aina tofauti na mimi na nimekuwa nikiendana nao, kwa mfano Yahya Tumbo na hivi sasa Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Mrisho Ngassa na Jamal Mnyate, wote wapo poa tu.

    Swali: Kocha gani bora zaidi kuwahi kufundishwa naye?

    Bocco: Makocha wengi walionifundisha wamenijenga sana na siku zote nawaona bora sana kwangu, kwani toka nilipotoka chini naamini wao ndiyo siri ya mafanikio yangu haya ya sasa, kwani wengi walinijenga niwe mshambuliaji wa kati na si pembeni na makocha wote wananitumia hivyo. Pia wananipa vitu tofauti na vya kisasa zaidi.

    Swali: Bao gani ambalo ni bora zaidi umewahi kulifunga?

    Bocco: Nimekuwa nikifunga magoli mengi magoli kama unafuatilia mechi zangu utagundua hilo na mabao ninayofunga ni yale yanayofungwa na washambuliaji asilia. Msimu uliomalizika nilifunga mabao ya kuvutia sana na hakika ulikuwa msimu bora sana kwangu.

    Swali: Ipi unadhani ilikuwa mechi bora zaidi kwa upande wako?

    Bocco: Kila mechi ilikuwa bora sana kwangu kwani kila ninapokuwa uwanjani nawaza kuipatia timu yangu ushindi, zile nilizofunga ndizo zilikuwa bora zaidi kwangu kwa sababu malengo yangu yalitimia.

    Swali: Kikosi gani bora ambacho uliwahi kukichezea?

    Bocco: Kwa kweli kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars na timu yangu ya Azam FC, kwani zote huwa tuna kikosi bora sana, ukweli huwa nafurahi nikiwepo katika timu zote mbili.

    NB: Mahojiano haya nilifanya na Bocco mwaka 2011 na yanapatikana katika lililokuwa jarida namba moja la mpira wa miguu nchini number10-Toleo la 17-La mwisho kutolewa.

      Current date/time is Sun May 19, 2024 5:07 pm