Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

Haji Manara atokwa na povu baada ya kulipuliwa na Abdi Banda

Haji Manara atokwa na povu baada ya kulipuliwa na Abdi Banda Empty Haji Manara atokwa na povu baada ya kulipuliwa na Abdi Banda

Post by MO SALAH on Tue Apr 10, 2018 11:04 am

Haji Manara atokwa na povu baada ya kulipuliwa na Abdi Banda Hqdefa10
Kama ilikupita hii.....Povu la Manara kwa Abdi Banda mchezaji wa zamani wa simba anayechezea Baroka fc ya south Africa


" Kumjibu mtu mjinga ni kufanana nae..ila kumwelimisha mjinga ni kumsaidia

Nimeona hyo video ya Salehe Ally na mchezaji wa Baroka fc (Kama nimeiandika vema )ya nchini Afrika kusini Abdi Bhanda

Bhanda alipata kuichezea klabu ya Simba kabla ya kujisajili na timu yake mpya
Kwenye video hyo Bhanda anaulizwa swali na mwandishi ni kitu gani hutatamani kikutokee ktk career yako ya kucheza Soka.. akajibu.jambo nisilotaka kuja kuntokea ni kwa viongozi waliopewa dhamana kuchukua mamlaka ya kwenda kuongea na vyombo vya habari huku wao hawana mamlaka hayo..huku akikiri kuwa kuna watu wameajiriwa kwa kupewa hyo mamlaka.

Halafu akaendelea kwa kuponda kwa mfano wangu eti kulalamikia maamuzi ya refarii aliochezesha mchezo wetu wa Ligi kuu baina yetu na Yanga..mchezo ulioisha kwa sare ya bila kufungana..
Mchezaji huyo alienda mbali zaidi kwa kusema jambo hilo linasababisha mpira wetu usiende mbele..

Nimjuze kwanza wajibu wa kazi yangu..mm ndio msemaji rasmi wa klabu ya Simba na nimepewa hyo mamlaka kama alivyosema yy mwenyew ktk interview yake..nikiongea mm naongea kwa niaba ya kamati ya kamati ya utendaji wa Simba..siongei jambo ila uongozi umeridhia na ndio maana kwa kipindi chote ambacho nipo Simba haijatokea hata kwa bahati mbaya mm kupishana kauli na viongozi wenzangu..
Hvyo dogo aelewe ile ni mamlaka yangu.

Pili mm kwenda kulalamikia maamuzi yale ni stand ya klabu na sikukurupuka kama alivyokurupuka yy ambae hata hajui nani msemaji rasmi wa klabu ya Simba..nimwambie kuanguka kwa mpira kuna sababu nyingi nchini na sio kulalamikia waamuzi pekee..hata huko South unapoomba Mungu watu hulalamikia waamuzi na walalamikaji ni viongozi,mashabiki,makocha na hata wachezaji.

Pia asisahau kulalamika kwangu ndio kulimsaidia asifungiwe adhabu kubwa na TFF baada ya kumpiga George kavila wa Kagera Sugar,hali iliopelekea kupata fursa ya kucheza Cosafa cup ambapo akaonekana na kusajiliwa huko South..

Nimkumbushe pia kulalamika kwangu ndio kulikopelekea utetezi ktk shauri lake kwa uongozi wa Simba ambapo alikuwa afukuzwe timu kitambo kwa kukosa nidhamu na maadili ya kambi..tena nilifanya utetezi mbele ya Bi mkubwa wake na bwana Bosnia ambae ni kama mlezi wake
Na hapo sitaki kumkumbusha huo ulalamishi wangu ulivyomnusuru yy ktk lile shauri lake la jinai..

Nimalizie kwa kumwambia weka akiba dogo..bado hujafika kokote wala usijione ushakuwa Abedi Pele au Lucas Radebe..huwa nazisikia tambo zako mbalimbali ukihojiwa na media za Tanzania..wakati mwingine ukibeza hata ulipotoka!!

Sijui ungekuwa ww ndio Samata ingekuwaje?
Sijawahi kumsikia Samata kwa njia yoyote akiponda hadharani viongozi wa bongo wala Simon Msuva au Ulimwengu..ila ww uliohamishia mpira mdomoni..jifunze kwa waliokutangulia na ujiwekee malengo yako ili ww,familia yako na Taifa kwa ujumla wafaidike,kupambana na mtu mwenye taaluma ya kuongea na kuandika ni kututafuta muhali tukaja kuongea yasioandikika...."
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 10:28 pm