Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.

Join the forum, it's quick and easy

Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.

Soka Sports

Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

4 posters

    Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger

    dembele
    dembele
    Junior Member


    Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger Empty Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger

    Post by dembele Tue Apr 10, 2018 12:06 pm

    kwanza nimeeleza kwamba sasa ni wazi Wenger anaondoka msimu huu. Kwenye post ntaonyesha dalili zinaonyesha Thomas Tuchel ndiye anachukua nafasi yake.

    1. Usajiri wa Obemeyang na Mkhitarian

    Si kawaida kwa Wenger kusajiri mchezaji mwenye miaka 29. Na si kawaida kabisa kwake kusajiri wachezaji wawili wenye umri huo kwa dirisha moja. Auba anakaribia miaka 29 na Miki amefikisha umri huo. Mwanzoni ilisemekana ni usajiri wa Mislintant lkn ulikuwa ushauri wa Tuchel au ulifanyika kumshawishi ajiunge na Arsenal kwa sababu alifanya nao kazi Dortmund.

    2. Uthibitisho wa Bayern Munich

    Bayern wamethibitisha kwamba walikuwa wanamuhitaji lakini amesaini na klabu nyingine. Matthaus akaenda mbali na kuitaja Arsenal. Si Arsenal wala Tuchel aliyekanusha madai hayo.

    3. Kauli ya Steve Bould

    Labda kuna watu wana wasi wasi kwamba Arsene Wenger kwa roho yake ngumu hatakubali kuachia ngazi. Wiki hii Wenger alikuwa na matatizo ya koo hivyo mkutano na waandishi wa habari alifanya msaidizi wake Steve Bould. Alipoulizwa kama Wenger atakuwepo alisema "ningependa iwe hivyo". Mtu kama Bould wa pili toka kwa Wenger angekuwa anajua boss wake atakuwepo angejibu 'definitely'.

    4. Thomas Tuchel kuikataa Bayern Munich

    Bayern Munich wao wenyewe wamethibitisha hilo. Wengine wanashangaa 'eti' kuikataa Bayern akaenda Arsenal. Hivi kocha mwenye miaka 44 anaenda pale kuongeza nini? Kama ni Bundesilga wanachukua kila mwaka na Champions League si kombe geni. Watu mliwahi kujiuliza kwa nini Guadiola aliondoka Barcelona na na Bayern? Unashinda kila kitu lakini watu wanaona kawaida

    5. Kauli ya Ikay Gundogan

    Kiungo wa Man City Gundogan ambaye alicheza chini ya Tuchel Dortmund alisema anasikia boss wake huyo anakuja Uingereza. Sidhani kama Gundogan anasikia kama sisi, anaweza kuwa ashaongea naye.

    6. Ataichagua Arsenal badala ya Chelsea

    Kuna fununu kwamba hata Chelsea wanamuhitaji. Kwangu mimi zaidi ya fedha sijui kama Chelsea bado inawavutia makocha wenye malengo ya muda mrefu. Chelsea wamewafukuza Mourinho, Anceloth, De Matteo na sasa wanakaribia kufanya hivyo kwa Conte mwaka mmoja baada ya kuchukua ubingwa. Binafsi huwa nadhani waliua kabisa carrier ya De Matteo. Mtu aliyewapa Champions League ktk historia ya kilabu wakati makocha wakubwa kama Mourinho, Schorali na Anceroth wamepita pale na wameshindwa hakutakiwa kutendewa vile.
    Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger Gettyi10
    Sandoka
    Sandoka
    New Member
    New Member


    Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger Empty Re: Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger

    Post by Sandoka Tue Apr 10, 2018 12:30 pm

    Arsene wenger hawezi kuiacha arsenal atastaafu palepale,
    Klabu ya arsenal hususa ni wamiliki wanapata faida kubwa sana kwaajili ya huyu kocha
    joker
    joker
    New Member
    New Member


    Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger Empty Re: Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger

    Post by joker Tue Apr 10, 2018 12:35 pm

    Sandoka wrote:Arsene wenger hawezi kuiacha arsenal atastaafu palepale,
    Klabu ya arsenal hususa ni wamiliki wanapata faida kubwa sana kwaajili ya huyu kocha

    Kuna kila dalili kuwa Arsenal wenger ataondoka mwishoni mwa msimu huu
    Nani
    Nani
    Junior Member


    Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger Empty Re: Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger

    Post by Nani Tue Apr 10, 2018 11:19 pm

    hatupendi kuona babu wenga akiondoka tutammisi sana EPL

    Sponsored content


    Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger Empty Re: Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger

    Post by Sponsored content


      Current date/time is Thu May 09, 2024 1:59 am