Soka Sports

je, bado hujawa member?

ni rahisi kuwa mwanajukwaa wa sokasports click register kutengeneza account yako.
itakuchukua sekunde 30 tu.
Soka Sports

Jukwaa La Wanamichezo Tanzania www.sokasports.forumotion.com

FIFA WORLD CUP CHAMPONS 2018 FRANCE .

  • Post new topic
  • Reply to topic

Chris Mauki amtaka Waziri awachukulie hatua Nandy na Bill Nas

Anonymous
salome
Guest

Chris Mauki amtaka Waziri awachukulie hatua Nandy na Bill Nas Empty Chris Mauki amtaka Waziri awachukulie hatua Nandy na Bill Nas

Post by salome on Fri Apr 13, 2018 3:33 pm

Chris Mauki amtaka Waziri awachukulie hatua Nandy na Bill Nas Nasii

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na mshauri wa masuala mbalimbali ya mahusiano Dr. Chris Mauki amefunguka na kutoa maoni yake kuhusu sakata la wasanii Nandy pamoja na Bill Nas kufuatia kuvuja kwa video yao wakiwa faragha.

Mauki ameitaka Wizara inayohusika na masuala ya sanaa ichukue hatua dhidi ya wasanii hao ili kudumisha maadili na nidhamu katika jamii hususani kwa wasanii ambao ni kioo cha jamii na kusewa endapo watafanya hivyo basi litakuwa funzo kwa wasanii wengine na watu wengine katika jamii.

"Mheshimiwa waziri Mwakyembe, Naibu Waziri pamoja na baraza la sanaa chini ya ndugu Mwingereza. Tutaiona nia yenu ya dhati kabisa kwenye kudumisha maadili na nidhamu katika jamii na hususani kwa wasanii ambao wanajiita "kioo cha jamii" pale ambapo hamtoinyamazia hii hali ya kuanikwa mitandaoni matukio ambayo kiuhalisia yalihitaji privacy, ninasimama sehemu ya ndugu zao hao wahusika, sehemu ya wazazi wao, sehemu ya wadogo zao, na wengine wengi ambao waliwaona kama role models wao. Kulikoni majukwaani tuwaone kama vioo vya jamii na huku nyuma mitandaoni mnaiharibu kabisa ile picha mliyoichora machoni pa watanzania"

Aidha Mauki aliendelea kusisitiza kuwa "Kama ilivyoenea katika public basi tujulishwe katika public ni hatua gani za kinidhamu zinafuata na onyo kwa wengine wenye fikra finyu na chafu kama hawa wanaohalalisha tabia za kingono mitandaoni. Masikio ya wenye akili na hekima yanasubiri kusikia kutoka kwenu viongozi wetu wenye mpini" alisisitiza Chris Mauki
  • Post new topic
  • Reply to topic

Current date/time is Fri May 24, 2019 10:29 pm